GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
We jamaa utakua choko,c bure
Siyo tu choko Mkuu bali ni ' choko choko ' kabisa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We jamaa utakua choko,c bure
Bro nenda kashtaki FIFA Yanga ishushwe daraja.Kwa Kipa mla ' mlungula ' maarufu Hussein Shariff a.k.a Casillas ningeshangaa sana leo Yanga kama isingeshinda magoli kuanzia 3 na hata hadi 10 na nimeshangaa kuona Yanga imewafunga hawa Kagera Goli chache hizo 6 tu. Kwa kuanzia kabla sijamjadili hapa Kipa Shariff ambao Binafsi ni ' Mshkaji ' na huwa tunakumbana sana katika ' Mabonanza ' Leaders na huwa tunaonana mno Mitaa ya Magomeni katika ' Ndondo ' ambazo huwa anacheza sana na kule Kwake ' Kigamboni ' pia huwa tunakutana sana tu.
Jiulizeni ni kwanini Simba Sports Club ilimuacha na ni kwanini alipogundulika tu amechukua ' Mlungula ' katika mechi baina ya Timu moja ' Tajiri ' ila kwa sasa inasuasua kwa kufungwa magoli tena ya kutokea katikati ya Uwanja akaanza kuwekwa ' Benchi ' ndipo Kijana Manyika Peter Jr akaanza kupata nafasi. Muulizeni baada ya kubanwa katika changing room siku hiyo alisema nini na baadae ' umafia ' gani Simba iliufanya kwa hiyo Timu na hadi leo hiyo Timu inaiheshimu Simba.
Hivi unategemea nini kama tu Kocha wa Kagera Sugar ' Mnafiki ' Mecky Mexime ni Mwana Yanga tena wa kufa Mtu? Tunajua jinsi Mecky alivyokuwa akichukuwa ' mizigo ' katika mechi mbili ambazo Timu yake ya Zamani ya Mtibwa Sugar ilicheza na Yanga hadi wakawa ' maadui ' za Kocha msaidizi wake Zubeiry Katwila.
Kama mlitizima mpira wa leo Yanga ilipitia katika upande wa Kushoto ambako huyo Beki aliyepangwa leo na Kagera Sugar ni Mwana Yanga hadi yupo hata tayari kutolewa ' Kafara ' na Yanga ili ishinde. Tunajua ' mzigo ' wa leo huko Kagera alipewa Kocha Mecky na yeye akausambaza kwa Mwana Yanga mwingine Beki Godfrey Taita na mwingine akausambaza kwa huyo ' Dogo ' Beki wa Kushoto na akahakikisha kuwa leo Mchezaji kama Themi Felix hampi nafasi na hata kama angempa basi angepewa ' maagizo ' maalum.
Mchezo wa leo ilikuwa tayari imeshapangwa kuwa Yanga ishinde tena kwa idadi kubwa ya ' Magoli ' ili tu kuweza ' Kunogesha ' Mkutano Mkuu wa dharura ambao ulikuwa ufanyike Kesho ila bahati nzuri Mahamaka huwa ' haitakagi ujinga ' imeusitisha hadi tarehe 24 November 2016 baada ya kugundua ' janja janja ' ya ' Gabachori '. Nia kubwa ya ' Kuwahonga ' leo Kagera Sugar na ifungwe goli nyingi ni kuweza kuwaaminisha wana Yanga ambao wengi wao ' hawajielewi ' katika ' mitima ' yao ili walewe ushindi na Kesho Mkutanoni kila kitu kiwe ' ndiyo ' na ' hewala hewala ' Kisha Mwanamume apewe ' Nembo ' na ' Timu ' yake ale atakavyo kwa miaka 10 kisha akimaliza aidai Yanga Tsh 98 billion kutoka hizi Tsh 11 billion anazowadai sasa.
Mwisho naomba niwaulizeni hivi hawa Kagera Sugar wa leo ndiyo wale waliocheza na Simba Sports Club wiki mbili zilizopita ambapo walikuwa ' wanahaha ' uwanja mzima huku wakicheza kwa nguvu na ari huku wakiwa na hasira na hamu ya ushindi ila wote wakatulizwa na ' Fundi ' Kichuya? Nawaombeni kwa umakini wenu rudieni kupitia mechi ya leo kisha angalieni ' magoli ' ya Yanga hasa la pili na la tatu kisha mwangalieni Golikipa Hussein Shariff Casillas wa Kigamboni alivyodaka ' kimlungula mlungula ' hadi ' Mnafiki ' mwenzie Kocha wake Mecky Mexime akaona ' noma ' na kumtoa ili ' kuzuga '.
Siku TAKUKURU wakisema waingie rasmi kuchunguza mechi za VPL hasa zinazoihusu Yanga FC nadhani nchi ' itatikisika ' kwa aibu kubwa kwani tunaoujua mpira wa ' Bongo ' kindaki ndaki hatushangai na ushindi wa ' Kimagumashi ' wa Yanga katika mechi zake ila watajitahidi lakini kwa Simba Sports Club ya safari hii ' watasubiri ' sana. Na Kesho karibuni ' Shamba la Bibi ' muweze kuona ' mauaji ' ya Karne ya ' Shalubela ' iyakayokumbana nayo Watoto wa ' Wakodishwaji FC '.
Kungekuwa kuna Kombe la Dunia la ' Kuhonga ' nadhani Klabu / Timu ya Yanga FC kila mwaka ingeibuka mshindi na pengine hata kukabidhiwa Kombe moja kwa moja. Naomba niishie hapa Tafadhali na namsubiri ' Mshikaji ' wangu Kipa wa Kagera Sugar Hussein Shariff Cassilas wa Kigamboni arudi mjini ili tukatanue sana na ' Mibia ' Kijiweni ' migo migo ' Baa maarufu ya Jirani kwa Marehemu Sheikh Yahya Hussein na zitakazobaki tutaenda zetu ' kubai ' nyuchi Uwanja wa Nyumbani Brazil Pub Tegeta mbele tu kidogo ya Kibo Complex.
Mechi zinaanza lini jamani?Nimemiss pressure za VPL kinoma.ligi emerejea. tusubir matokeo ya viwanjani maana kelele za magazeti zilizidi
LeoMechi zinaanza lini jamani?Nimemiss pressure za VPL kinoma.
Naomba ratiba kama hutojali tafadhali.
Ligi Kuu Bara 2016/2017 Fixtures - Soccer/TanzaniaNaomba ratiba kama hutojali tafadhali.
Asante [emoji120]
Ubarikiwe mkuu [emoji120]