Vpl leo tar 13/09/2015 Uwanja wa Taifa, Yanga vs Coast Union saa 10:00 Jioni

mkolaj

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2014
Posts
3,023
Reaction score
1,089
Katika muendelezo wa ligi kuu Tanzania Bara, leo katika uwanja wa taifa patakuwa hapatoshi pale miamba wa soka tanzania Dar Young Africans watakapokuwa wenyeji dhidi ya timu ya coast union kutoka mkoani Tanga.
Coast wataingia uwanjani leo huku wakikumbuka kipigo cha magoli 8-0 kutoka kwa Wanajangwani hao msimu wa 2014/2015.
Yanga iliyofanya usajili mkubwa msimu huu kwa kuwaleta wachezaji hatari kabisa akina Donald Ngoma, Thaban Kamusoko, Deus Kaseke, Vicent Bosou, Winga hatari Georfrey Mwashiuya na wakali wengine kibao wana hamu kubwa ya kutaka kuwaonyesha coast mpira wa kiholanzi na kuwahakikishia kuwa msimu uliopipta hawakubahatisha kuwachukulia point zote 6 katika michezo yote miwili.

Kocha mkuu wa Yanga ametamba kuibuka na ushindi katika mchezo wa leo huku akijiamini na safu yake ya ushambuliaji chini ya Donald Ngoma na Mrundi Amissi Tambwe.

Kuwaletea haya yote kutoka uwanja wa Taifa utakuwa nami nkolaj sambamba na Makoye Matale, cnjona, bantu lady, na wanajangwani wengine tuliomo humu jukwaani.

Hapa ni michezo tu mwanzo mwisho, siasa peleka ikulu.

................. Full Time.........
...............YANGA 2-0 COAST UNION.......
 
Mbona sio mahala pake hapa!!!!!!!!!
 
Makoye Matale nitakuwepo kama kawa. Yanga timu - piga Coastal Union bao za kutosha ili tukwee kwenye usukani wa ligi.
 
Last edited by a moderator:
Makoye Matale nitakuwepo kama kawa. Yanga timu - piga Coastal Union bao za kutosha ili tukwee kwenye usukani wa ligi.
Yanga timu imara, viongozi imara, benchi la ufundi imara na mashabiki imara.
Timu yanga tupigie hao coast goli nyingi za kutosha, ikiwezekana fanya nusu ya msimu uliopita.
 
Last edited by a moderator:
kwakuwa leo mvua imenyesha Dar, Coastal anashinda bila wasiwasi wowote. Ukibisha basi wewe kipaji
 
kwakuwa leo mvua imenyesha Dar, Coastal anashinda bila wasiwasi wowote. Ukibisha basi wewe kipaji

Mikia kwa imani za kishirikina mnatisha! Mvua inyeshe isinyeshe kipigo kwa Coastal Union hakiepukiki.
 
Yanga timu imara, viongozi imara, benchi la ufundi imara na mashabiki imara.
Timu yanga tupigie hao coast goli nyingi za kutosha, ikiwezekana fanya nusu ya msimu uliopita.

.... na watu wote waseme AMINAAAA!
 
kwakuwa leo mvua imenyesha Dar, Coastal anashinda bila wasiwasi wowote. Ukibisha basi wewe kipaji
Kwenye timu ya Coast mvua inakuwa mchezaji wa namba ngapi!!!!!!?
Labda hiyo mvua iwe inacheza golini inaweza kuwazuia yanga kupitisha mpira golini, tofauti na hapo kipigo kwa Coast Union hakiepukiki.....
 
Yanga Bingwa piiiiiigaaa hao Simba B
 
Kikosi cha timu ya Yanga kinachotarajia kuanza msimu mpya wa ligi kuu leo tar 13/09/2015........
1.Ally Mustapha "Barthez"
2.Mbuyu Twite Junior
3.Hajji Mwinyi Ngwali
4.Nadir Haroub Cannavaro
5.Kelvin Yondan Vidic
6.Thaban Kamusoko
7.Simon Msuva
8.Haruna Niyonzima
9.Amissi Tambwe
10.Donald Ngoma
11.Geofray Mwashiuya

Kocha mkuu Hans Van Der Pluijm

Kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa

Meneja wa timu Afidhi Saleh

Daktari wa timu Juma Sufiani.

Kila la kheir timu ya wananchi Dar Young Africans.

Ushindi lazima leo dhidi ya Coast Union.
 
Kifo chatangazwa cha Kosto Yunioni kitakachotokea jioni hii katika uwanja wa Taifa. Mazishi yatafanyika hapo hapo uwanjani.

Habari ziwafikie Julio wa Wachimbaalmasi FC, Kerr wa Mikia FC, Hall wa Lambalamba FC pamoja na ndugu na jamaa wote wenye vinasaba vya Mikia FC, Makoye Matale anawapa pole wafiwa wote na anamtakia marehemu mapumziko ya amani popote atakapokuwepo.
 
Last edited by a moderator:

kikosi dhaifu kabisa ukanda huu wa africa mashariki na kati, coasta union 2 yanga 1
 
Msitake kutuchafulia jukwaa. Kama anataka urais wa Obama akagombee Marekani. Hapa ni soka mwanzo mwisho
 
Kwenye timu ya Coast mvua inakuwa mchezaji wa namba ngapi!!!!!!?
Labda hiyo mvua iwe inacheza golini inaweza kuwazuia yanga kupitisha mpira golini, tofauti na hapo kipigo kwa Coast Union hakiepukiki.....

Kwa Yanga ipi? hii ya Gita au Ngoma??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…