VPL, leo tar 24/04/2015 YANGA AFRICA VS RUVU SHOOTING_Live updates...............

Hata wangeongezewa mabeki mia! Yanga ni Mabingwa 2015! Hakuna wa kumzuia mwaka huu!!!

Masao Bwire akiongea na RFA amedai kuwa 'Yanga ni gari bovu lililokata breki halafu limekuwa likizuiwa na vigingi dhaifu', akaongeza kuwa 'Ruvu Shooting ni kigingi imara kitakachozuia hilo gari bovu'. Amejinasibu kuwa endapo wataifunga Yanga watajipatia heshima kubwa na kutambuliwa na Watanzania kwani Yanga ndiyo inaongoza ligi kwa sasa.

Swali linabaki kuwa: je, ni kweli Ruvu Shooting ni kigingi imara kwa Yanga?
 
Anajifariji tu! Lakini pia anaji contradict maana mara anaiponda kwa kusema gari bovu lisilo na break na mara anasema wakiifunga Yanga watasifiwa maana Yanga inaongoza ligi ! Wasemaji wetu hawa wanahitaji kwenda shule pia!
 
Hii yanga mmeahidiwa mnafunga ngapi maana ilishachezwa eti...
 
Unamkumbuka yule beki aliyemkaba Tambwe?? Leo tena uso kwa macho tena kaongezwa beki mwingine kwaajili ya Msuba aah Msuva

Hata mabeki wa Mgambo waliomkaba Okwi kule Tanga na kusababisha Simba kucharazwa bao 2-0 juzi pia walikuwepo na kushuhudia kichapo cha 4-0 kutoka Simba.

Ruvu Shooting waelewe kuwa hizi mechi za mwisho siyo sawa na mechi za mwanzo!
 
Hii yanga mmeahidiwa mnafunga ngapi maana ilishachezwa eti...

Mkuu ndetichia, wewe ni mnazi wa Azam na tunaheshimu uamuzi wako kama binadamu mwingine yeyote. Hata hivyo kauli kama hizi zinaharibu taswira ya soka kwa watu kuanza kuhisi kuwa mechi zinachezwa nje ya uwanja. Nafahamu kuwa ungependa kuona Yanga siyo tu ikitoa sare bali ikipoteza kabisa mchezo wa leo kwa maslahi ya timu yako.

Sisi kama Yanga hatujui tutapata bao ngapi, tunachojua ni kuwa tutapata pointi 3 muhimu.
 
Last edited by a moderator:

kwanini Salvatore walimuondoa hapo kwenye benchi la ufundi
 
Hata mabeki wa Mgambo waliomkaba Okwi kule Tanga na kusababisha Simba kucharazwa bao 2-0 juzi pia walikuwepo na kushuhudia kichapo cha 4-0 kutoka Simba.

Ruvu Shooting waelewe kuwa hizi mechi za mwisho siyo sawa na mechi za mwanzo!

andelea kujipa moyo
 

nafasi ya kipa imebadilishwa, sasa ataanza batez.
 
 
sisi tunamaliza ligi, eti wao ndo wanaanza ligi..
 
Ni kweli Dida ni tatizo sana bora ya Bathez! Akishindwa kudhihirisha ubora wake leo basi tena!
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba kipa Deogratius Munishi dida ameondolewa kwenye kikosi cha yanga kitakachoanza leo dhidi ya ruvu shooting na nafasi yake imechukuliwa na kipa Ally Mustapha "Barthez".

YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…