VPL: Simba SC Vs Azam FC


Mkuu pamoja na kwamba tunakubaliana wote kuwa soka ni mchezo wa amani,Upendo

Ndio essence ya Fair Play.Nakataa kabisa watu kuumizana kwa faulu zisizo za kimpira na waamuzi wasifanye kitu

Kitu ninachokipinga katika suala lenu la Tambwe ni kwamba limeamuliwa kisiasa.....Maamuzi yale yangefanywa bila kukurupuka...ripoti ya kamisaa ingesubiriwa.

Kwa minajili hiyo maaamuzi yale yalifanywa kwa kuzingatia picha mnato kwenye gazeti la championi tu.Picha mnato haziwezi kusema kila kitu.

Maamuzi ya kukurupuka kwa sababu tu Yanga wamelalamika.

Na hicho ndicho Sisi watu wa Simba tuakipinga
 
Refa alishindwa kumudu mchezo kwa 99%...

Mkuu nashindwa kuelewa eti kwamba maamuzi yalifanyika kabla ya ripoti ya kamisaa. Ninayo clip ya StarTV kupitia SimuTV ya Vodacom inayoeleza wazi kuwa maamuzi hayo yalifikiwa baada ya kuridhika na ripoti ya kamisaa. Kama umejiunga na SimuTV hebu jaribu kuisikikiza hapa:

http://simu.tv/7pCaZ2N
 

Huwezi kushangilia mchezaji kumfanyia faulo mchezaji mwingine, hatukatai ni kweli kuna faulo za kiuanamichezo lakini si faulo za kukusudia kumuumiza mwenzako tena kwenye sehemu za mwili ambazo ni sensitive na zinaweza kusababisha kifo au mchezaji kupooza. Hivi ikitokea mchezaji kapooza au kufa kwa sababu ulimgonga kwenye spinal cord au kwenye medulla oblongata na team yako ikashinda au ikachukua kombe huo ushindi au hilo kombe litakuwa na thamani gani kwako huku kila mara unakumbuka kwamba ulisababisha mchezaji mwenzako kupooza au kufa?
 

Mkuu umeongea kiutu uzima sana. Asante sana Mkuu.
 
Kuhusu suala la Tambwe, Bodi ya Ligi walikurupuka kutoa maamuzi ya haraka kabla hata kupata maelezo ya kamisaa wa michezo.. eti kisa Yanga katishia kujitoa katika ligi!!
Game ya Yanga na JKT Ruvu ilichezwa tarehe 17/01/2015 ,gazeti la Jumatatu (19/01/2015) la Champion likaonyesha ile picha ya Tambwe ,Jioni Yanga wakatoa malalamiko yao kupitia kwa Msemaji wao.Adhabu ya refa kufungiwa imetangazwa 23/01/2015.Kosa limefanyika tarehe 17 adhabu imetolewa tarehe 23 (siku ya sita baada ya tukio).Labda ungetusaidia report ya kamisaa inawasilishwa TFF baada ya muda gani na game imechezwa hapa Dar ?


Bodi ya Ligi inatakiwa iwaamini viongozi inaowateua kusimamia mechi kama makamisaa, marefa, n.k.. tofauti na hali ilivyo sasa ya kupuuza ripoti za makamisaa
Game ya Simba vs Azam sidhani kama unahitaji report ya kamisaa wakati refa anaonekana kabisa alichemsha
Hao makamisaa ndio wanachangia sana kuharibu soka letu,kama wangekuwa waandika yanayotokea uwanjani marefa wengi sana wangefungiwa,inakuwaje inafikia wakati refa anawaogopa wachezaji? Wachezaji wanacheza rafu refa anawaangalia tu,marefa wa bongo hawazungumzi na wachezaji kuwaonya.Ulaya wachezaji wakisukumana refa anawaita na kuongea nao huku kwetu hakuna hicho kitu
 
Tunakoelekea hata waamuzi wa ligi zetu itabidi FRAT ikodishe au iruhusu wawekezaji wa kutoka nchi za nje hasa Ulaya walete waamuzi Tanzania.
Inavyoonesha tumeshindwa kabisa kupata waamuzi wa soka wenye sifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…