VPL: Simba SC Vs Azam FC

VPL: Simba SC Vs Azam FC

wadau karibuni uwanja wa taifa kuona mechi kali tangu mwaka 2015 uingie vijana wa unyamani simba sc watakipiga na kinara wa ligi kuu Azam fc wana lambalamba, vijana wa simba chuo cha soka Tanzania wameahidi kutoa dozi kulingana na hali ya mgonjwa kwa kupiga mpira mwingi ili kupata points 3 muhimu, simba itakuw inawategea vijana waliokwiva kama nahodha isihaka hassani, jonas mkude, saidi ndemla, ramandani singano, okwi(mtoa roho), saimon serenkuma, uku Azam fc ikiwategemea kipre tchetche, domayo, kavumbagu, bocco na brian majegwa.
Karibuni wadau wote mtapata update hapahapa jf.
Mechi itaanza saa kumi kamili jioni
Team today
1. MWADINI ALI
2. SHOMARI KAPOMBE
3. ERASTO NYONI
4. AGGREY MORIS
5. PASCAL WAWA
6. BOLOU MICHAEL
7. MUDATHIR YAHYA
8. FRANK DOMAYO
9. DIDIER KAVUMBAGU
10. KIPRE TCHETCHE
11. HIMIDI MAO
AKIBA
1. KHALID MAHADHI
2. SAID MORAD
3. GADIEL MICHAEL
4. KELVIN FRIDAY
5. KHAMISI MCHA
6. AMRI KIEMBA
7. JOHN BOCCO

Weka na kikosi cha mnyama ili tutoe tathmini.
 
Azam hana madhara kwenu wakati anaitafuta pointi ya 23 wakti nyinyi mna 18?
Ama kweli mtu aliyekata tamaa utamjua tu.

Azam atakuwa mbele kwa mchezo mmoja Mkuu, usikonde, mbio za Azam ni sawa na mbio za panya sakafuni ambazo huishia ukingoni. Nyie chezeni mpate matokeo yoyote sisi ndio wababe wa hii ligi. Hili siyo kombe la mapinduzi eti!

Haingii akilini hata kwa wale wa Milembe eti timu iko nafasi ya pili tofauti ya pointi mbili halafu mashabiki wakate tamaa, ikiwa hawa watakata tamaa itakuwaje kwa wale ambao timu yao iko nafasi ya 9 pointi 8 nyuma ya vinara?
 
Mimi naomba tu mtoke draw ya bila kufungana.
Simba mna roho mbaya sana, leo timu yenu inacheza mnaomba mfungwe!!!!!. Ili tu Azam iendelee kuwa top, lazima mtakuwa wanga loh.
Siye tuna points 18 na tumecheza michezo 10, tumeanza na Mungu tutamaliza na Mungu.
 
Azam naichukia, Simba nayo siipendi. Sijui leo niwe upande upi! Azam akishinda bado hana madhara kwetu. Simba naye hata akishinda bado si lolote na si chochote.

Leo niko neutral, matokeo yoyote na yaje tu. Mwenyezi Mungu aitendee haki kila timu kwa kuvuna ilichopanda.

Mkuu Makoye Matale mimi hata siku moja siwezi kuiombea Simba mafanikio iwe ndani au nje!!!

Naiombea Azam ishinde hiyo mechi kwa sbb hata wao tukicheza na Azam huwa wanaishangilia leo najikodisha mimi mwenyewe kwa dk 90 baaada ya hapo siwataki!!
 
Last edited by a moderator:
Azam Leo inapiga mnyama,ngoja nisogee kibanda umiza nikakae sit I ya Mbele kabisa
 
makoye Leo hakuna visingizio vya taulo wala gloves.Leo hakuna uchawi.Leo ni mpira tu

Mkuu naomba nikukumbushe kuwa niliwahi kupost hapa jamvini kuwa Yanga ndio tageti la uchawi katika soka. Kila kitimu kinachoanzishwa kinataka kuifunga Yanga kwani ndiyo SI unit katika soka la bongo (usibishe!). Sina lengo la kushabikia uchawi maana ni aibu hata kuutaja tu kwa jina lake ingawa kweli uchawi upo. Kwa Yanga muda wote iko cautious kweli kweli!

Ngoja nirudie kwa manufaa ya wengi:

DOUGLAS Muhani, beki wa zamani aliyepata kuchezea klabu kadhaa za Tanzania pamoja timu ya taifa, Taifa Stars, anakumbuka siku ambayo yeye na wachezaji wenzake walipokesha makaburini wakiroga ili kupata ushindi.

Hii ilikuwa ni mechi ya Ligi ya Taifa Tanzania katika kituo cha Mwanza mwaka 1978, wakati akiichezea Sigara (sasa Moro United) na mechi hiyo ilikuwa inaikutanisha timu yake na Yanga.

"Tuliambiwa na mtaalamu wetu kutoka Tanga kwamba lazima tufanye ndumba kwa sababu mechi ingekuwa ngumu. Mganga wetu, ambaye tulikuwa naye tangu mwanzo wa mechi zetu, alituambia kwamba tungeshinda, lakini mwenzetu mmoja angedondoka uwanjani.

"Tuliamriwa kutomgusa wala kumsogelea, kwa sababu kufanya hivyo kungemaanisha kwamba angepoteza maisha," anakumbuka. "Na kweli, kabla hatujafunga bao, mchezaji mwenzetu, John Mlebo, alianguka na kuzimia. Tulimtazama tu mpaka alipochukuliwa kwenye machela. Tulifunga bao, na wakati tulipodhani tumeshinda, Omar Hussein akaisawazishia Yanga zikiwa zimesalia dakika nane tu."

Muhani anasema katika maisha yake ya uchezaji, akiwa amechezea klabu kadhaa kama Sigara, Coastal Union, Maji Maji na Bandari Mtwara, amekumbana na matukio mengi ya ushirikina kuelekea mechi za soka.

Anasema kuchanjwa chale kwenye vifundo vya miguu, kujifukiza ubani, kuoga maji yaliyowekwa talasimu pamoja na kuvalishwa hirizi ni mambo ya kawaida aliyokumbana nayo na ambayo anasema yanaendelea kufanyika kwa siri katika timu nyingi za soka, siyo Tanzania tu, bali Afrika kwa ujumla.

Source: Imani za uchawi zinavyoangamiza soka, nini kifanyike kwa sasa? - Fikra PevuFikra Pevu
 
Mchawi mara nyingi asipofanikiwa kitu cha kwanza kuona ni kwamba anafanyiwa uchawi, wewe unafikiri wachezaji na mashabiki na viongozi pia kama sio wachawi hizo akili za kwenda kuchukua taulo, kuchukua gloves na kwenda kufukua fukua uwanjani wanazitoa wapi?
 
Makoye Matale acha kupaka rangi upepo.anayeamini ushirikina ni mshirikina
 
Last edited by a moderator:
mimi ni mshabiki wa mnyama. ila leo ningependa AZAM washinde ili wasogee mbele na kuipa YANGA wakati mgumu zaidi kipoint. Simba tumejitoa kwenye kombe hili maana halina faida sana kama la nani mtani Jembe.lile lina pesa nying zaidi kuliko hata VPL. so leo hata AZAM Wakishinda sitajisikia vibaya sana kwa kuwa YANGA hawatakuwa na amani. na mimi ninachotaka ni YANGA kutokuwa na furaha maisha yao yote. TEAM YA WASHIRIKINA KAMA YANGA ilipaswa ifungiwe lakini naona TFF inawatizama tu.

Mkuu unafahamu kwamba Jamal Malinzi ana kadi ya yanga. Ukitaka yanga ifungiwe ni sawa na kusubiri embe dodo lianguke chini ya mwarobaini.
 
Mchawi mara nyingi asipofanikiwa kitu cha kwanza kuona ni kwamba anafanyiwa uchawi, wewe unafikiri wachezaji na mashabiki na viongozi pia kama sio wachawi hizo akili za kwenda kuchukua taulo, kuchukua gloves na kwenda kufukua fukua uwanjani wanazitoa wapi?

Mkuu nimesema Yanga tuko cautious muda wote! Hebu angalia mwaka 1978 kabla Azam wala Mtibwa hazijazaliwa Yanga tayari walikuwa wanarogwa, kwa nini wasichukue tahadhari?

Wewe mwenyewe unajua Gamboshi jinsi inavyoshikilia 'balimi' kibao waliofariki kimiujizamiujiza, kitu gani Mkuu kinakufanya ushangae vijiuchawi vidogovidogo uwanjani?
 
Baba yetu uliye mbinguni nakuomba uwajalie azam ushindi katika mechi hii dhidi simba, ili mtumishi wako niwe na amani siku ya leo.... AMEN

Kumbe wakina Steve yanga wengine wapo. Maana ukimuuliza Steve katika maisha anaogopa nini zaidi, atakwambia Washabiki wa Simba.
 
Nawaona simba ukawa kwa mbaaaali wamekuja hapa taifa ili kuhakikisha kuwa simba wanapata sare ama kufungwa.
 
Mkuu nimesema Yanga tuko cautious muda wote! Hebu angalia mwaka 1978 kabla Azam wala Mtibwa hazijazaliwa Yanga tayari walikuwa wanarogwa, kwa nini wasichukue tahadhari?

Wewe mwenyewe unajua Gamboshi jinsi inavyoshikilia 'balimi' kibao waliofariki kimiujizamiujiza, kitu gani Mkuu kinakufanya ushangae vijiuchawi vidogovidogo uwanjani?

Hiyo cautiousness ipo kwa sababu na nyie mko hivyo, hiyo habari ya Gamboshi ni myth tu ndo maana kila mtu atakwambia nilisimuliwa hakuna aliyewahi kushuhudia au kufika huko Gamboshi akajionee kama tunavyosikia, ingawa kuna kijiji kina jina hilo na ni kijiji kama vijiji vingine vya Tanzania. Siku zote mwizi anakuwa yuko cautious kuhusu kuibiwa.
 
Back
Top Bottom