VPL: Simba v Prisons 28-02-2015

kazi kucheza na Adobe Photoshop. Sawa waliifunga Yanga tano lakini watasubiri kushiriki mashindano ya CAF kwa miaka mitano.
Kweli yanga hamnazo mnafungwa 5-0, 3-1, 2-0, kwa miaka mitatu mfululizo, mnaongoza bao 3 mpaka half time, kutokana na litimu lenu kuwa dhaifu mpaka muhonge ndio lishinde zinarudi zote bado mnasema Adobe Photoshop! Kateni rufaa TFF basi maana mmefungwa kwa Adobe Photoshop na sio Soka la dimbani.
 
Wakitoa Suluhu tu, hawaonekanagi humu majukwaani.
Join Date : 2nd January 2015
Location : Tanzania
Posts : 263
Rep Power : 361
Likes Received88
Likes Given88


Hahahahaaa....inashangaza mtoto wa chekechea ambaye bado anatoka makamasi na kuyalamba akafahamu ratiba na mahudhurio ya baba zake vijiweni. Haya ni maajabu mengine ya dunia.
 

Kumbe unakubali kuwa Simba "jahazi linazama" a.k.a kiwango "kimeshuka". Cha kushangaza ni kwamba yanga mpo kwenye kiwango cha hali ya juu kwa standard yenu ila mmetuacha point 8 tuu, na sisi ni wa 3 ktk msimamo! Sipati picha treni letu likipamba moto mziki utakuaje.
 
Miaka yote mitatu ukiacha ule muziki mkubwa wa Simba uliowapiga 5 bila 2012, yanga wamekuwa wakipangiwa chipukizi wa kutoka timu ya Simba B na kwa kiwango chao hicho hicho wanachojisifia wamekuwa wakidhalilishwa kwa vipigo tu.

Wana nini cha kujivunia mwaka huu ambacho miaka yote 3 hawakuwa nacho kama si ushamba wa kula makombo wanayotupa Simba tu. Liangalie litimu lao karibia nusu ni makapi ya Simba kwanini tusiwapige tu. Mbinu zao akina Yondani tunazijua Okwi na Messi wanapita kama highway wakati yeye anabakia kushika jezi na kucheza faulu za kijinga.

Huyo Barthez tunamfahamu tumfungie angle gani kama ilivyokuwa kwa Kaseja na hiyo ndiyo itakuwa mechi yake ya mwisho kupangwa kama walivyofanya kwa Kaseja. Ngassa tunamfahamu ni mbio tu akiweka na mtu beki roho mbaya hafurukuti, Amis Tambwe tunamuelewa uchezaji wake ni mpaka apikiwe ndipo afunge akifungiwa njia ya mpira anabaki kulia na marefa tu, kama aliogopa kukabwa koo sasa atakabwa miguu.
 

Mkuu, mbona unakua mvivu kufukiria kwa kutumia Brain..!

Ile post yangu haikumlenga mtu mmoja tu.! Bali iko general...

Nilicho maanisha ni kwamba wengi wao wa mashabiki wa Simba sports club... huwa hawanaga habit ya ku-engage katika thread zinazo husu timu yao. Bali huwa wanasuburi timu yao ishinde ndipo wanakuwa active sana kwenye thread za aina hizi.

Punguza hasira zako..!
Nadhani jibu lako ni la kishamba kidogo. Unadhani kuwa join date ya mtu.. ndicho kithibitisho cha ufuatiliaji wa mijadara mbalimbali humu JF.

Nimekuwa humu ndani kama "GUEST" (nikiwa kama mpitiaji na msomaji wa uzi na comments nyingi tu) kwa kipindi kirefu sana.. Kabla ya kuamua ku-join jf. Hivyo posting behavior za watu wengi humu ndani nazitambua vyema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…