VPL: Simba VS Majimaji FC, Simba yairarua Majimaji bao 4-0 uwanja wa Taifa

Omog Huko Aliko Lazima Ajitafakari Upya Mbinu Zake....
Massoud Djuma hongera aisee! Mzungu lazima Afate System Yako tu ya Mfumo ulioujenga.
Yaani Nikuwa Pale Uwanjani Masoud Akukukaa Kwenye Kiti Mpaka Mpira Unaisha.Muda Wote Anawapa Maelekezo Vijana Wake ..
Na Yupo Karibu Sana Na Wachezeji Naona Kabisa Ile Connection Na Wachezaji Safi Yake Sana.
Mi Nimempenda Bure Yale Magori Ya Leo Nilitamani Kama Nikamuhug Yeye.
 
Kwa kweli timu inaonekana ina amani, wachezaji wote.
Hofu yangu ni akipona majeruhi Niyonzima, kwa kweli hapa itabidi apangwe mtu aliye kwenye kiwango, ma sasa ni Ndemla ktk hiyo namba.
 
Magoli aliyofungwa kipa wa Azam jana?
Nyuma ya pazia katika mpira w Tanzania ukifunuliwa utashangaa sana mambo yanayifanyika. Mechi ya Yanga na Majimaji usiku was mkesha makomandoo was Yanga wakizuiwa kwenda kumwaga ndumba usiku was manane uwanja wa Majimaji zikapigwa ngumi mpaka ffu wakapelekwa
 
Naona hata mzungu ni kutumalizia hela tu,Djuma atosha kweli
 
Tulipo wasajili John Bocco na Shomari Kapombe baadhi walibeza mno usajili huo. Ila sasa yamkini wanaelewa


Ukweli Ni Kwamba Baada Ya Kuwasajili Hawa Mashabiki Wa [HASHTAG]#Ndala[/HASHTAG] Kwa hule wivu wao tu Wakaanza Kasumba kama Walivyoanza Kwa Okwi Kumwita Mzee..

Na Bahati Mbaya Kuna Wale Washabiki Wa Simba Wanaoangalia Mpira [HASHTAG]#JamiiForum[/HASHTAG] badala Ya [HASHTAG]#Uwanjani[/HASHTAG] au Kwenye [HASHTAG]#Television[/HASHTAG] Wakaanza Kusikiliza Propaganda Za Ndala na Kuanza Kuleta Dharau Juu Ya Bocco na Kapombe.
 
Hii Ya Uwanjani Jana Kuna Muda Bocco alikosa Goli Yeye Na Kipa Akapaisha Kuna Watu walikaa nyuma yangu Izo Lawama Walizompa Bocco Baada ya Kufunga la kwanza na La pili Nikaona Wanabadirisha Maneno. Na Ile pasi Alompa Okwi Nikaona Wanaimba Kabisa Bocco Bocco...Ikabidi Niwacheke Tuuh
 
Hakuna jambo la ajabu kumfunga majimaji Taifa... Ngoja uende kwao ukiwa unahitaji ushindi kwa udi na uvumba huku Yanga anakupumulia kwa point moja na mechi moja mkononi.


Hata Kwa Kagera Sugar mulisema Kuwa Tukikanyaga Kwenye Home Ground Yao Tutakiona hatimae Mwisho Wa Mchezo Mukapoteana... πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…