VPL: Super Saturday 17/10/2015

VPL: Super Saturday 17/10/2015

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
18,960
Reaction score
67,654
Leo ndio leo katika soka la Bongo, Mabingwa wa Tanzania Vs Mabingwa wa Kagame, yaani Yanga vs Azam fc pale Uwanja wa Taifa. Hapa Ngoma pale Pascal Wawa, Kule Kipre Tchetche huku Cannavaro. Dakika 90 ndio mwamuzi wa yote pale Taifa.

Kule Mbeya, wenyeji wa Jiji hilo, wagonga nyundo wa Mbeya City uso kwa macho na Mnyama Mkali wa Mwituni, Simba Sc katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine. Huku Boban kule Kiiza. Tukutane saa 10.
==========

Yanga Vs Azam FC
00' Mpira umeanza kati na walioanzisha ngw'e hii ya kwanza ni Azam FC
40' Azam wanapata kona kuelekea Yanga, hata hivyo kona hio iliyopigwa na Farid ilitoka nje yenyewe.
41' Yanga wanapata kona baada ya mabeki wa Azam kuchanganyana, kona hio ilipanguliwa na Manula.
43' Beki wa Yanga anafanya kazi ya ziada kuondoa mpira ulioingizwa kati kumfikia mshambuliaji wa timu pinzani.
45+2':A S soccer: Yanga wanapata goli la kwanza, Goli lililofungwa na Donald Ngoma kutokana na pasi nzuri kutoka kwa Juma Abdul.
45+3' Mpira umeingia mapumziko

45' Baada ya mapumziko, timu zimerejea kwa ajili ya ngw'e ya mwisho ambayo itaamua mshindi ama suluhu.
48' Azam wamekosa goli baada ya piga nikupige langoni mwa Yanga
52' Himid Mao wa Azam FC anapewa kadi ya njano baada ya kucheza mchezo usio wa kiuungwana
54' Malimi Busungi anakosa goli baada ya kupiga shuti kali langoni mwa Azam hata hivyo hakuweza kulenga goli.
61' Yanga wanacheza vizuri langoni mwa Azam baada ya mchezo mzuri kutoka kwa Ngoma lakini mpira wa Msuva ulizuiwa na Manula.
63' Wanga anatoka na nafasi yake kuchukuliwa na Kipre Tchetche.
70' Frank Domayo anachukua nafasi ya Michael timu ya Azam FC
72' Faulo kuelekea Yanga baada ya Kamusuko kumzibia njia mchezaji wa Azam
73' Kipre Tchetche anapiga juu ya goli nafasi ya faulo aliyopata
79' Saidi Juma anaingia kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite aliyeumia
81' :A S soccer:Kipre Tcheche anasawazisha baada ya mpira mzuri kutoka kwa Farid uliompoteza beki wa Yanga.
84' Yanga wanapata penati baada ya Simon Msuva kupambana na Manula na wachezaji wa Azam wanamzonga mwamuzi.
87' Aishi Manula anapewa kadi ya manjano
88' Manula anapangua penati hivyo matokeo yanabakia suluhu ya 1-1
89' Aishi Manula anaondoa hatari kwa mpira ulianzia kona na anagaagaa chini ikiwa ishara ya kuumia.
90+4'Shomari Kapombe anapewa kadi ya njano
90+5' Manula yuko chini baada ya kuondoa mpira ulioanzia kwenye adhabu ndogo.
90+6' Mwamuzi anapuliza kipenga kuashiria mwisho wa mchezo.

Yanga anabakia kileleni kwa kukusanya pointi 16 akifatiwa na Azam mwenye pointi 16 pia wakitofautiana magoli.
========

Update Sokoine
:A S soccer:Mbeya City 0-1 Simba Sc
Goli lilifungwa baada ya kona kupigwa, mpira uligongwa kichwa na Jonas Mkude aliumalizia nyavuni akimuacha goli kipa wake wa zamani, Juma Kaseja akigaagaa.


 
Last edited by a moderator:
Kila la kheri Azam Fc
Kila la kheri Mbeya city
Kila la kheri Majimaji
 
Azam leo kukiona cha moto taifa,simba ahhhh wapigwe tu huko sokon,DAIMA MBELE NYUMA MWIKO
 
Yanga 3-1 Azam fc

Mbeya city 2-1 Simba
 
Nina wasiwasi kiungo ya yanga bila fundi niyo, nadhani azam watamiliki dimba sanaaa
 
yanga najua haiwezi kuniangusha tatizo hawa Chelsea
 
Nina wasiwasi kiungo ya yanga bila fundi niyo, nadhani azam watamiliki dimba sanaaa

mwenzako nashukuru kutocheza leo, maana hizi big mechi anadengua sana, sasa leo ndo utawajua vizuri akina TELELA, KASEKE, KAMUSOKO.. hapo MAKAPU hajavuruga mfumo wa Stewart.
 
Ebwana nimeota yanga tumepigwa 3-0. Ila nakataa katika jina la yesu iwe vice versa is true.
 
mechi ya ligi kuu vodacom itakayoanza saa 16:00 kati ya YANGA SC Vs AZAM FC - U/TAIFA.
KIKOSI CHA YANGA LEO. 1.Ally Mustafa Mtinge "Barthez" 2.Juma Abdul Jaffary. 3.Haji Mwinyi Ngwali Makame.
4.Kelvin Patrick Yondani "Cotton" 5.Nadir Ally Haroub "Cannavaro"
6.Mbuyu Junior Twite. 7.Salum Abo Telela 'Master'
8.Thaban Scara Kamusoko 'Rasta' 9.Donald Dombo Ngoma.
10.Amiss Jocelyn Tambwe.
11.Malimi Ahmed Busungu.
SUB. Deogratius Munishi 'Dida'
Vicent Bossou
Juma Said Makapu Andrey Countinho Saimon Happygod Msuva
Deus David Kaseke. Anthony Mattheo. BENCHI LA UFUNDI. Kocha Mkuu. Hans Van Der Pluijm Kocha Msaidizi. Juma Mwambusi. Meneja. Hafidh Saleh. Daktari. Juma Sufiani KILA LA HERI YANGA AFRIKA.
 
Sina shaka kabisa na Mnyama mkali wa Mwituni.. Naimani leo ataendeleza maangamizi kama kawaida yake.
 
Back
Top Bottom