VPL Yanga vs Prisons live update 16 September 2015

VPL Yanga vs Prisons live update 16 September 2015

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
14,804
Reaction score
10,715
Leo ligi kuu ya Tanzania, VPL inaingia mzunguko wa pili. Yanga SC wanawakaribisha maafande wa prisons toka Mbeya. Ikumbukwe kuwa katika mechi yao ya awali, Prisons walitakata vilivyo licha ya kubanjuliwa magoli mawili kwa moja na Azam FC. Yanga nao waliwafundisha soka wateja wao Coast Union kwa kuwatandika mabao mawili kwa nunge na kujikita kileleni mwa ligi. Hivyo Tutarajie mtanange wa kasi uliosheheni ufundi mwingi na hivyo kutoa burudani Safi kwa mashabiki na wapenzi wa kabumbu. Karibuni

Final results :
Matokeo ya Vpl katika viwanja mbalimbali leo tar. 16/09/2015.

Yanga 3-0 Prisons

Jkt Mgambo 0-2 Simba

Maji maji 1-0 Kagera suger

Mbeya city 3-0 Ruvu star

Stand United 0-2 Azam fc

Toto Africans 1-2 Mtibwa suger

Ndanda 1-0 Coast Union

Mwadui 2 - 0 African Sports
 
Leo ligi kuu ya Tanzania, VPL inaingia mzunguko wa pili. Yanga SC wanawakaribisha maafande wa prisons toka Mbeya. Ikumbukwe kuwa katika mechi yao ya awali, Prisons walitakata vilivyo licha ya kubanjuliwa magoli mawili kwa moja na Azam FC. Yanga nao waliwafundisha soka wateja wao Coast Union kwa kuwatandika mabao mawili kwa nunge na kujikita kileleni mwa ligi. Hivyo Tutarajie mtanange wa kasi uliosheheni ufundi mwingi na hivyo kutoa burudani Safi kwa mashabiki na wapenzi wa kabumbu. Karibuni

mzunguko wa pili???anywy yanga piga hao warembo
 
KIKOSI CHA YANGA LEO VS PRISONS 1.Barthez 2.Twite 3.Mwinyi 4.Canavaro 5.Yondan 'Vidic' 6.Kamusoko 'Davis' 7.Msuva 'Pedro' 8. Niyonzima'Fabrigas' 9.Ngoma 'Martial' 10.Tambwe 'Benzema' 11.Kaseke 'Iniesta'
 
Huyu jamaa namfahamu kuwa ni Mwana CCM, lakini pia nafahamu fika kuwa yeye si Mwana Yanga hivyo Yanga sio CCM.

Hivyo basi Deo Corleone wewe ni muongo!
 
Attachments

  • Rage.png
    Rage.png
    7.8 KB · Views: 733
Match nyingine zitakazopigwa leo katika viwanja mbalimbali Jijin Dar es salaam na mikoani ni:-
Yanga vs Prisons- Dar es salaam
Jkt Mgambo vs Simba- Tanga
Maji maji vs Kagera suger-Songea
Mbeya city vs Ruvu star- Mbeya
Stand United vs Azam- Shinyanga
Toto Africans vs Mtibwa suger- Mwanza
Ndanda vs Coast Union- Mtwara

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mchezo mmoja kati ya Mwadui fc dhidi ya African sports ya Tanga.

Michezo yote kuanza saa 10:00 kwa saa za Afrika Mashariki.

Kila la kheir timu ya wananchi Dar Young African, lakini pia naitakia ushindi timu ya KUKAYA Mtwara timu ya Ndanda dhidi ya Wagosi wa kaya Coast Union.
 
Back
Top Bottom