Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,804
- 10,715
Leo ligi kuu ya Tanzania, VPL inaingia mzunguko wa pili. Yanga SC wanawakaribisha maafande wa prisons toka Mbeya. Ikumbukwe kuwa katika mechi yao ya awali, Prisons walitakata vilivyo licha ya kubanjuliwa magoli mawili kwa moja na Azam FC. Yanga nao waliwafundisha soka wateja wao Coast Union kwa kuwatandika mabao mawili kwa nunge na kujikita kileleni mwa ligi. Hivyo Tutarajie mtanange wa kasi uliosheheni ufundi mwingi na hivyo kutoa burudani Safi kwa mashabiki na wapenzi wa kabumbu. Karibuni
Final results :
Final results :
Matokeo ya Vpl katika viwanja mbalimbali leo tar. 16/09/2015.
Yanga 3-0 Prisons
Jkt Mgambo 0-2 Simba
Maji maji 1-0 Kagera suger
Mbeya city 3-0 Ruvu star
Stand United 0-2 Azam fc
Toto Africans 1-2 Mtibwa suger
Ndanda 1-0 Coast Union
Mwadui 2 - 0 African Sports