Vunja Bei aambiwa 'Thank You,' Sandaland apewa kazi ya kuuza Jezi za Simba

Undugu utatuua kwenye masuala muhimu, Simba SC kila nikiimgalia huwa nachoka. Nasema hivi sio kishabiki.

1. Mo Dewji, amepewa timu bila upingamizi au uuzwaji wa Hisa kwa kushindania na wawekezaji wengine. Hii ilipaswa kurekebishwa haraka kwa sababu hakuna muda Mo aliwahi ipatia Simba Pesa Bure, mara zote ametoa katika win win situation.

2. Usambazaji wa Jezi, kwa miaka na miaka ulikuwa chini ya Kaka/Baba yake kupitia Sunderland. Figisu nyingi amefanyiwa Vunja bei, ila ashindwe kusambaza kujustfy ndugu huyo kuwa alipaswa kupewa tenda. Na sasa amepewa tena ndugu wa Mo Dewji.

3. Africarries ni ya Ndugu wa Mo, nayo imeingia mkataba na Simba.

4. MO Foundation, MO Extra nk, hii inawanyima haki wafanyabiasha wengine kupewa nafasi ya kutangaza biashara au kupartner na hii timu.

5. Fatma Dewji, naye amepewa Simba Queen.

Pamoja na madhaifu ya Yanga ila angalau kwenye Mikataba ya Matangazo ipo kwa watu tofauti tofauti na wasio ma uhusiano wa kibiashara. GSM, TAIFA GAS, AFYA, SPORTPESA ni tofauti kabisa kidogo HIER yuko na uhusiano na GSM.

Kwa maendeleo ya Mpira wetu hili tulipige vita kwa nguvu zetu zote.
 
logo yake ya vunja bei ilikua kubwa kuliko nembo ya club alafu akaihamisha kutoka chini had kuja Katikati ya kifua ili ionekane haraka
 
na Mbet ni ndugu wa mo pia?
 
Magazine wa mahesabu na fifisufigusu zote za soka ni fifa mwenye hila aendee fifa simba ishushushwe daraja ila simba nachoomini kwa niaba ya wanachama tuko vizuri hadi muda huu hamna kochi aloonyesha kututoka
 
GSM, TAIFA GAS, AFYA, SPORT PESA ni tofauti!?

Mkuu, Fanya kufukunyua, utajua hao wote jambo lao moja, hapo wamefanya Portifolio tu. ila muhusika ni Ji Esi EM in umbrella of mr smile.
 
Mimi ni Simba ...uko sahihi kabisa
 
umenena vyema kabisa.muhindi uwa apendi ushindani.
 
Shida ikwapi kama wamefika bei. Sisi wanasimba tunaheshimu na kuappreciate mchango wa mo kama utopolo wanavomtukuza garib kwa sasa.

Halafu hao taifa gas ndio hao hao gsm kwa mgongo wa nyuma wa msoga
 
Shida ikwapi kama wamefika bei. Sisi wanasimba tunaheshimu na kuappreciate mchango wa mo kama utopolo wanavomtukuza garib kwa sasa.
Wamefika bei walishindana na nani? Wewe ulisikia hiyo tenda? Uwepo usawa wa kibiashara, zile ni timu za Umma sio binafsi, watu wanachangia michango yao.
 
Mmiliki wa Simba sio Mo Dewji ni Wanachama
2. Usambazaji wa Jezi, kwa miaka na miaka ulikuwa chini ya Kaka/Baba yake kupitia Sunderland. Figisu nyingi amefanyiwa Vunja bei, ila ashindwe kusambaza kujustfy ndugu huyo kuwa alipaswa kupewa tenda. Na sasa amepewa tena ndugu wa Mo Dewji.
Vunjabei amejitahidi ila alishindwa, Uto inapata sh ngapi kwa kila Jersey?
3. Africarries ni ya Ndugu wa Mo, nayo imeingia mkataba na Simba.
Una ndugu mwenye ubavu akachukue nafasi ya Africarriers?
4. MO Foundation, MO Extra nk, hii inawanyima haki wafanyabiasha wengine kupewa nafasi ya kutangaza biashara au kupartner na hii timu.
Ni bidhaa zinazohitaji kutangazwa na Mo tayari Simba ni platform yake kubwa
5. Fatma Dewji, naye amepewa Simba Queen.
Hajapewa, Fatema yupo kama influencer tu
Pamoja na madhaifu ya Yanga ila angalau kwenye Mikataba ya Matangazo ipo kwa watu tofauti tofauti na wasio ma uhusiano wa kibiashara. GSM, TAIFA GAS, AFYA, SPORTPESA ni tofauti kabisa kidogo HIER yuko na uhusiano na GSM.
Afya ni watercom
Taifa gas ni Rostam
Sportpesa wakenya.

M-bet
Air Tanzania
Emirates Aluminium
Hawa wote ni wakwenu?
Kwa maendeleo ya Mpira wetu hili tulipige vita kwa nguvu zetu zote.
Piga wewe na watu wakwenu
 
DP World wana sponsor sana michezo tofauti tofauti nchi nyingi. kwao wana sponsor mpaka Michezo ya fedha nyingi sana.

Nawaonea gere Yanga.

Mama Samia anaupiga mwingi Kimataifa.
 
Hivi kabla mo hajajitokeza simba hao wawekezaji wengine walikuwa wapi kuichukua timu mpaka utake competition?

Yanga alipojitoa manji ilichukua muda gani kumpata gsm? Gsm wenyewe mama alisema hawabani means kwa kiasi kikubwa wapo pale kwa kimchongo tu.

Lesson: nchi yetu hawapo wawekezaji wa kutupa pesa kwenye mpira wakategemea faida so hao waliopo tuwashukuru sana. Au uliwahi peleka tangazo pale simba ukanyimwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…