Undugu utatuua kwenye masuala muhimu, Simba SC kila nikiimgalia huwa nachoka. Nasema hivi sio kishabiki.
1. Mo Dewji, amepewa timu bila upingamizi au uuzwaji wa Hisa kwa kushindania na wawekezaji wengine. Hii ilipaswa kurekebishwa haraka kwa sababu hakuna muda Mo aliwahi ipatia Simba Pesa Bure, mara zote ametoa katika win win situation.
2. Usambazaji wa Jezi, kwa miaka na miaka ulikuwa chini ya Kaka/Baba yake kupitia Sunderland. Figisu nyingi amefanyiwa Vunja bei, ila ashindwe kusambaza kujustfy ndugu huyo kuwa alipaswa kupewa tenda. Na sasa amepewa tena ndugu wa Mo Dewji.
3. Africarries ni ya Ndugu wa Mo, nayo imeingia mkataba na Simba.
4. MO Foundation, MO Extra nk, hii inawanyima haki wafanyabiasha wengine kupewa nafasi ya kutangaza biashara au kupartner na hii timu.
5. Fatma Dewji, naye amepewa Simba Queen.
Pamoja na madhaifu ya Yanga ila angalau kwenye Mikataba ya Matangazo ipo kwa watu tofauti tofauti na wasio ma uhusiano wa kibiashara. GSM, TAIFA GAS, AFYA, SPORTPESA ni tofauti kabisa kidogo HIER yuko na uhusiano na GSM.
Kwa maendeleo ya Mpira wetu hili tulipige vita kwa nguvu zetu zote.