Vunja Bei aambiwa 'Thank You,' Sandaland apewa kazi ya kuuza Jezi za Simba

Wamefika bei walishindana na nani? Wewe ulisikia hiyo tenda? Uwepo usawa wa kibiashara, zile ni timu za Umma sio binafsi, watu wanachangia michango yao.

We jamaa unaongea kama hushirikishi ubongo wako.
hivi wewe umewahi kupeleka matangazo yako pale simba wakagoma kukuwekea?

Kabla ya mo kuja, simba si ilikuwepo? Kwa nini hawakwenda kupeleka matangazo yao pale?

Timu ni za umma sawa hao wenye timu wanamchango gani kwenye timu? Manji aliwaachia timu yanga, uliona kilichotokea? Mambo mengine muwe na shukrani na sio kuleta ubishi usio na msingi.
 
Wewe umewahi kutaka kuwekeza nini pale simba ukashindwa?.au unazungumzia ela za wenzako?
 
Wawekezaji Wengi wapo wanasubiri aondoke Tu waingie

hebu wataje wachache unaowafahamu.

kabla hajaingia mo wao walikuwa wapi?
Yanga alipojitoa manji ilichukua muda gani kutulia?
Kwa nini nchi yetu timu zenye connection na watu wakubwa serikalini ndo zinawadhamini?

Kama timu zetu zingekuwa na faida kibiashara kwa wawekezaji kuja basi baada ya manji kujitoa ilipaswa tusikie yanga ikigombaniwa lakini hali halisi tuliona. Na hata mwekezaji aliyepo mama kasema juzi kuwa anambeba. kwa hiyo unaweza ona mazingira ya connection na michongo hapo.

Ukweli ni kwamba huyu mo inabidi ashukuriwe tu.
 
DP World wana sponsor sana michezo tofauti tofauti nchi nyingi. kwao wana sponsor mpaka Michezo ya fedha nyingi sana.

Nawaonea gere Yanga.

Mama Samia anaupiga mwingi Kimataifa.
Chawa huku ni michezo tu
 
Kwann nipeleke wakati hawajatangaza tenda ya jezi. Hujataka kuelewa basi niishie hapo.
 
logo yake ya vunja bei ilikua kubwa kuliko nembo ya club alafu akaihamisha kutoka chini had kuja Katikati ya kifua ili ionekane haraka
Duh saskuonekana kwa log ndio nn Wala hii siyo hoja kbsa ,ishu Ni undugulaizetioni ndani ya club hi kongwe kbsa baran africa
 
Kwann nipeleke wakati hawajatangaza tenda ya jezi. Hujataka kuelewa basi niishie hapo.

sasa kama wewe ni mwekezaji ungeona fursa hapo ungeenda mwenyewe. Ila kwa sababu wawekezaji wanajua hiyo ni biashara kichaa, ndio maana timu inalazimika kutafuta wawekezaji.
 
Duh saskuonekana kwa log ndio nn Wala hii siyo hoja kbsa ,ishu Ni undugulaizetioni ndani ya club hi kongwe kbsa baran africa
kapewa kazi kaishindwa mwenyewe kashindwa kuzalisha jezi kuendana na uhitaji, msimu mpya unaanza lakin mashabiki bado hawana jezi mpya, alaf bahati mbaya hadi mdhamini kashabadilishwa lakin mashabiki walishindwa kupata jez wakaendelea kuvaa za sportpesa.
ilitakiwa kwanzia siku ya Simba day mzigo upo wa kutosha ila ye alishindwa alichofanikiwa ni kubuni logo kubwa ya jina lake na kuiweka sehem inayoonekana kwenye jezi

jezi hazina ubunifu wowote hazivutii, ni Bora tu watu wabebane kuliko kuangalia usawa na kumpa mtu tenda wakati anashindwa kufikia matumaini ya mashabiki
 
Hata m beti nayo ni ya mo
 
Hakuna mwekezaji hapa duniani anawekeza kutoa sandakalawe,, kila uwekezaji lazima mwekezaji awe na lengo la faida,,,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…