Vunja Bei anaunga-unga, Simba msimpe mkataba

Vunja bei ni geresha tu tender ya kusambaza jezi MO ndio ameichukua. Tumlaumu MO na siyo vunja bei
 
Umeongea kitaalam sana. Big up
 
Huu ni ukweli mweupe. Acheni kumtetea aaibike ndo ataacha kuchukua tenda.
 
Kwani kuna tatizo gani ukiendelea kuishabikia Simba ukiwa umevaa nguo zako za nyumbani?
Ili mradi wachezaji wamevaa jezi mimi naona haina shida.
 
Vunjabei ni from ile jamii inauza mitumba hapo Kariakoo, angekuwa anatokea wale weusi wenzetu walio na hisa kubwa DSE na wamiliki wa LTD nyingi hapa bongo asingekuwa anafanya kazi kienyeji.
Mkataba mnono wenye uhakika wa faida anasumbua vile
Haya ndio maneno sasa.
 

Fact, umeongea ukweli, there is something unique na creativity kwa Jezi za Yanga.

Jezi za simba kwa kifupi ni za hovyo na wala sio za hovyo kidogo, hazifai.
 
Binafsi jezi za Yanga pamoja na wengi kuzisifia sipendi kabisa design zake. Mimi ni mpenzi wa classic look ambayo timu nyingi za Ulaya bado wanatumia ambayo ni simple plain color ikiwa na mistari fulani sehemu ya jezi. Siyo mbaya kuwa na kit moja yenye maurembo mengi kwa ajili ya kutumika kwenye mechi zinazochezwa siku za sikukuu.

Kasoro ambazo ningezitoa katika jezi za sasa ni 3. Kwanza kuongeza wepesi wa material za kitambaa. Pili ni kupunguza size za logo kuanzia ya Simba na ya kit supplier (hizi zimekuwa kubwa mno). Tatu ni maandishi ya main sponsor, nadhani trend sasa hivi jezi nyingi za nje, maandishi ya main sponsor ni madogo sana kwa hiyo logo ya M-BET ipunguzwe sana ukubwa wake. Ukubwa wa maandishi haumaanishi kuwa unaongeza ushawishi kwa watu.
 
Mkuu sasa tuna offer ya Adidas
 
Zipo timu za kujifunzia lakini sio Simba sc. Abaki Polisi Tz nk. Ajifunzie huko. Hata kwenye construction kuna miradi ya kukuza experience, huwezi kupewa Busisi Bridge from nowhere tu
 
Kuna ukweli hapa. Angalia namna vikaptula vinavyowashika wachezaji. Hata namna zilivyoshonwa ni kienyeji mno. Sijui haoni jezi na bukta za Azam au Namungo zinavyomwagika vizuri?
 
Kusema kweli kuna watu wengi wanahitaji jezi za quality za Simba lakini sio rahisi kuziona.
Ninawajua baadhi ya watu waliotoka huku mikoani walinunua jezi za yanga moja kwa sh elfu themanini( 80,000) kwa sababu ya quality.

Kuna watu fulani wajinga wanaona kutengeneza mijezi mingi mibovu ndio kuwajali wawapenzi wa Simba.Lakini ukweli ni bora jezi ziwe chache lakini za kiwango.

Hii nchi tupo wengi tu wenye uwezo wa kununua jezi ya elfu 60- laki.

Naunga mkono hoja,zabuni hii zipewe kampuni kubwa kwani wanunuzi tupo
 
WE UPO KUMBE!!1!
 
Huyo vunja Bei apumzishwe kwanza anatutesa mashabiki kuhangaika kugombania jezi kama vichaa
 
Huyo vunja Bei apumzishwe kwanza anatutesa mashabiki kuhangaika kugombania jezi kama vichaa
Nafikiri hana watalaamu wa supply chain and logistics, anaona kama kila mtu ni sagula-sagula. Imagine nilienda moja la duka lake kununua jezi zenye kola nikakuta hawana,lakini kila siku ana post anazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…