Vurugu kubwa zazuka bunge la Kenya

Vurugu kubwa zazuka bunge la Kenya

Wabunge wa Kenya wametofautiana vikali bunge na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.

Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.

Wabunge wa upinzani wlaipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.
141218101518_kenya_bunge__512x288_bbc_nocredit.jpg

Seneta Johnston Muthama alijipata pabaya kwnai long;i yake iliraruliwa katika mvutano bungeni humo

Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kuyaja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema 'bado mapambano.'

Spika wa bunge Justin Muturi wakati mmoja alimuru walinzi wa bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.

Mswada huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw augaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.
141218102025_muthama__512x288_bbc_nocredit.jpg

Seneta Muthama pia alijeruhiwa vibaya mguuni

Mapendekezo ya mswada huo ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali.

Pia ikiwa mswada huo utapistihwa kuwa sheria, mashirika ya habari yatatozwa faini ya hadili shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au picha ambazo zinaleta hofu na kusababisha taharuki.

Mswada huu umetolewa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Al Shabaab wakilalamika na kutaka wanajeshi wa Kenya kuondolewa Somalia
Rais Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo kuimarisha usalama wa tangui mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya kifahari la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.

Chanzo:BBC
 
Jamaa wamegoma na kuzua vurugu bungeni, hakuna tena cha ndi ama hapana, kama hoja ina matatizo haipitishwi ovyo. Nimeipenda hii, ila wataalamu watuelezee kwa utaratibu matatizo ya hii bill nini.

Last edited by a moderator:
10430485_394912697336973_3374932050406635666_n.jpg

Jubilee MPs Alice Wahome,Sakuda,Kimani Ngunjiri and Kiuna get into a figgt with CORD senators Muthama,Wetangula and Orengo

10014624_394912750670301_2390306813035363920_n.jpg

Hii inakuja kwenye bunge letu la budget, subirini tu
 
Kizaazaa cha aina yake kimeibuka Bungeni Kenya wakati muswada wa sheria ya ulinzi ulipokuwa unajadiliwa.Mapigano hayo yalisababishwa na kutupiana maneno makali kati ya serikali na wabunge wa upinzani.
Mapigano hayo yamesababisha spika wa bunge la Kenya Justin Muturi kuliahirisha bunge mpaka saa nane na nusu leo mchana.
Hii ni mara ya pili bunge la Kenya kuahirishwa wakati wa kujadili muswada huo.Muswada huo umeleta hisia kali mpya leo baada ya spika wa bunge kusoma sheria ya kufanya vurugu bungeni jambo lilippelekea wabunge kunyanyuka na kuanza kurushiana ngumi.
Katika vurugu hizo maseneta Moses Wetangula na Johnstone Muthama wa CORD walichaniwa nguo zao suruali na shati.Pia wabunge walichanachana muswada huo na kutupatupa hovyo karatasi bungeni.
Matarajio ni kwamba huenda bunge hilo lisioneshwa live wabunge watakaporudi hiyo saa nane na nusu ama likaahirishwa mpaka X-mass ipite.
Wenzetu wanapojadili maslahi ya nchi yao hawataki upuuzi hata kidogo.Unaweza ukaliwa nyama ukileta ujinga.
Kwetu Tanzania bado tunawabembeleza wezi wa Escrow waturejeshee mabilioni yetu kwa huruma zao wenyewe.
 
Attachments

  • muthama3.jpgnnn.jpg
    muthama3.jpgnnn.jpg
    34.2 KB · Views: 285
Wewe unataka kila kitu uige acha pumba!!
 
Kwani kupigana ndo akili?? Acha ujinga!
 
Hawa ndo wanaume, sio vibunge vyetu vyatanzania vinaendekeza mipasho tuu nakuitia ndio kila kitu.
 
hao ni zaidi ya tanzania ila kwa mwendo huu ipo siku na tz itafka huko
 
Hapa inabidi zipigwe ndio kutakua na kuheshimiana ...shwain ...kama wafuasi wenu mitaani hadi wanauliwa kwa kupigania haki....waheshimiwa na wao lazima wakubali suluba kidogo
 
[h=1]Mswada wazua zahma bungeni Kenya[/h]
  • Dakika 4 zilizopita
Mshirikishe mwenzako
Bunge la Kenya Wabunge wa Kenya wametofautiana vikali bunge na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.
Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani wlaipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.
Seneta Johnston Muthama alijipata pabaya kwnai long;i yake iliraruliwa katika mvutano bungeni humo Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kuyaja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema 'bado mapambano.'
Spika wa bunge Justin Muturi wakati mmoja alimuru walinzi wa bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.
Mswada huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw augaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.
Seneta Muthama pia alijeruhiwa vibaya mguuni Mapendekezo ya mswada huo ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali.
Pia ikiwa mswada huo utapistihwa kuwa sheria, mashirika ya habari yatatozwa faini ya hadili shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au picha ambazo zinaleta hofu na kusababisha taharuki.
Mswada huu umetolewa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Al Shabaab wakilalamika na kutaka wanajeshi wa Kenya kuondolewa Somalia
Rais Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo kuimarisha usalama wa tangui mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya kifahari la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.

Mswada wazua zahma bungeni Kenya - BBC Swahili
 
.... Hata Ukawa Wangekomaa Bungeni Na Kuzuia Katiba Ya Chenge Isiandikwe Hata Kwa Ngumi.!
 
naam mwakan ntakaposhinda ubunge kwa tiket ya chadema kutokea jimbo la mpwapwa naenda kui apply hyo, nataka wale waimba mipasho wa ccm kwenye mambo yeny maslahi mapana ya kitaifa wakileta mipasho itakua n mwendo wa ngumi tu kwenda mbele, jiandaeni kupata burudan hyo
 
Back
Top Bottom