Sahir Punzy
Member
- Jan 13, 2015
- 86
- 55
Vyombo vya Habari vimeripoti juu ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi lililongozwa na Godefroid Niyombare, meja jenerali mstaafu wa jeshi la Burundi kuipinduwa serikali ya Raisi Piere Nkurunzninza wa nchi hiyo. Jaribio hilo ni baada ya maandamano na mikwaruzano ya hapa na pale kwa wiki mbili mfululizo kufuatia tangazo la raisi wa nchi hiyo kuongeza muhula wa watatu wa uraisi. Jambo ambalo ni kinyume na katiba ya nchi hiyo na pia ni kinyume na Mkataba wa Amani wa Arusha. Jaribio hilo la Mapinduzi lilitokea wakati ambapo Raisi huyo yuko kikaoni jijini Dar es Salaam kutafuta suluhisho la mgogoro huo wa nchi yake. Maoni
Kinachojiri nchini Burundi katika upana wake kisiasa si zaidi, ila ni mvutano wa maslahi na kumakinisha athari ya kisiasa baina ya madola ya kibepari, hususan Marekani yenye ghera ya juu kumakinisha athari na ushawishi wake na kuhifadhi maslahi yake nchini humo kupitia mtu wake ambae ndio Raisi wa sasa Pierre Nkurunziza. Marekani inaonekana ina shaka juu ya mrithi wa kiti hicho baada ya Raisi huyo.
Na kwa upande mwengine, nchi za Ulaya, mabwana wakoloni wa asili wa nchi ya Burundi nao wana shauku kubwa ya kuirejesha tena nchi hiyo katika milki yao. Asili ya nchi ya Burundi ilikuwa pamoja na Rwanda, ikiwa nchi moja zama za ukoloni wa Ujerumani/German East Africa. Nayo ikiitwa Ruanda-Urundi. Baada ya kushindwa Ujerumani katika Vita vya Kwanza, ardhi hiyo ikanyanganywa Ujerumani na kupatiwa Ubelgiji iliyoigawa baina ya Burundi na Rwanda. Ubelgiji kwa maslahi yao ya kisiasa ndani ya Ruanda-Urundi ilimakinisha kwa kiasi kikubwa mgawanyiko mkubwa na chuki za kikabila baina ya Watutsi na Wahutu. Makabila mawili makubwa zaidi ya nchi hiyo. Hali hiyo ilipelekea kuripuka kwa husuma kubwa ya kikabila na mauwaji makubwa ndani ya mwaka 1959, ambapo Wahutu waliwavamia na kuwauwa Watutsi kwa maelfu.
Kufuatia nakama hiyo Watutsi wengi walikimbilia nchi za Uganda, Congo na Tanzania kutafuta amani ili kuwa mbali na balaa hilo. Mpaka leo nchi zote zilizopakana na Burundi na Rwanda zina jamii kubwa za makabila mawili hayo. Burundi, licha ya kuchukuliwa kuwa miongoni mwa nchi maskini mno duniani. Lakini ni nchi iliyobarikiwa rasilmali nyingi na mazingira ya hali ya hewa nyororo miongoni mwa nchi za eneo la Maziwa Makuu. Burundi ni mzalishaji mkubwa wa kahawa miongoni mwa nchi kumi zinazozalisha kahawa kwa wingi ndani ya Afrika. Na mmoja kati ya wateja wakubwa wa kahawa ya Burundi ni kampuni ya Starbucks Corp.
Aidha, kwa mujibu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Burundi ina Asilimia 6 ya hazina ya maadini ya nikeli kiulimwengu. Zaidi ya hayo, nchi hiyo ndio chanzo cha mto Nile ulipounganisha na Ziwa Victoria kupitia mto wa Ruvyironza. Pia kati ya maziwa makubwa ya Afrika Mashariki, Burundi imechukuwa sehemu kubwa ya Ziwa Tanganyika ndani ya eneo la pembe ya Kusini magharibi ya nchi hiyo. Ingawaje kiasili Raisi Pierre Nkurunziza wa Burundi sio Mtutsi. Lakini mara nyingi Marekani imekuwa ikitumia karata ya kikabila ili kumakinisha athari na ushawishi wake kupitia Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikitawaliwa na kabila la Watutsi walioungwa mkono na Maraekani tangu mwaka 1994.
Wakati waasi wa Kitutsi waliokuwa wakiungwa mkono na Marekani kushika hatamu za madaraka ndani ya Rwanda mnamo mwaka 1994. Na wale wa mashariki mwa Kongo, kwa kushirikiana pamoja na nchi hizi tatu walijenga ngome madhubuti kuhifadhi athari na ushawishi wa Marekani katikati eneo hili nyeti la Afrika. Na kwa hakika waliweza kuzuiya na kung'oa athari ya Uingereza na Ufaransa katika eneo hili. Ndio maana, wakati jaribio hili la mapinduzi likitokea dhidi ya Raisi wa Burundi. Msemaji wa Ikulu ya Marekani ya White House, Josh Earnest alitamka:

"Tunatoa mwito kwa pande zote kuweka silaha chini, kumaliza vurugu, na kufanya subra, kwa kuwa ni serekali ya Burundi ndio yenye mamlaka na dhamana ya kuweka masharti muwafaka yanayohitajika kufanya uchaguzi. Pia Josh Earnest aliongeza kusema kwamba Marekani bado inamtambuwa Raisi Nkurunziza kuwa ndio raisi halali.
Kwa hivyo, qadhia iko wazi kabisa kwamba Raisi Pierre Nkurunziza, yuko upande wa Marekani. Na inaaminika kwamba Meja jenerali Godefroid Niyombare, afisa wa jeshi mstaafu aliyeongoza mapinduzi, kilichopelekea kufutwa kazi na Raisi Pierre Nkurunziza ni baada ya kuvuja waraka wake wa kurasa kumi unaoelezea msimamo wake wa kutokubaliana na jaribio la raisi huyo kuongeza muhula wa tatu wa uraisi. Sambamba na hilo, mufakirina wa Ulaya wanalichukulia jaribio hilo la Mapinduzi ndani ya Burundi kuwa ni bishara njema sana: Fillip Reyntjens, Profesa wa Sheria na Siasa katika Chuo Kikuu cha Antwerp, Ubelgiji, akiwa pia Mtaalamu wa Masuala ya Ukanda wa Maziwa Makuu alisema:
"Ikiwa mapinduzi haya yatafanikiwa na kumakinika, yanaweza kuitwa kuwa ni mapinduzi yenye kheri kubwa"
Kwa hakika, chini ya minyororo ya mfumo wa kibepari, Afrika licha ya kubarikiwa kwa rasilmali nyingi na utajiri, bado linachukuliwa kuwa miongoni mwa mabara maskini wa kutupwa, duni na lililoshindwa kabisaa! Matokeo yake, wakaazi wake daima hubakia kuwa wahanga na medani ya mivutano ya kisiasa baina ya madola ya kibepari. Afrika ina kiu kali cha mfumo mbadala ili wakaazi wake wakombolewe kifikra na kuukomboa mrundikano mkubwa wa rasilmali zake ambazo huporwa kwa gharama duni kama si bure kamwe !