Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
1. UTANGULIZI
Mgodi wa Hadija Mkupi & Partners uliopo katika eneo la kijiji cha Msasa Runzewe Geita ulianza kufanya kazi mwishoni mwa mwaka 2025.
2. UENDESHAJI WA MGODI
Mgodi huu unaendeshwa kwa namna mbili ambapo wamiliki wa leseni wanachimba katika maeneo huku maeneo mengine wamewakabidhi wachimbaji wadogo (Wamiliki wa madaraja) kufanya kazi ya uchimbaji katika leseni zao kwa makubaliano maalum.
3. USIMAMIZI WA MAPATO YA SERIKALI
Shughuli za usimamizi wa mapato ya Serikali hufanywa na kamati maalum inayojumuisha maafisa toka ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Ofisi ya Madini pamoja na Ofisi ya Usalama na OCD.
Ukokotoaji wa stahiki za Serikali hufanywa kwa mujibu wa Sheria ya Madini Sura 123 ambapo baada ya uthamishaji asilimia zifuatazo hukatwa kama malipo ya stahiki ya Serikali:
- Asilimia sita (6%) mrabaha
- Asilimia moja (1%) ada ya ukaguzi
- Asilimia 0.1 (0.1%) HIV levy
Jumla ya stahiki za Serikali ambazo hukusanywa na TUME YA MADINI ni 7.01% toka kwenye uzalishaji uliofanyika.
NB: Zipo tozo nyingine kama Service levy 0.25% ambazo hutozwa na mamlaka nyingine za Serikali kama Halmashauri.
6. UPOTOSHAJI ULIOFANYIKA
Kumekuwa na taarifa za upotoshaji zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kwamba vurugu zinazotokea kwenye mgodi wa Msasa ni kwa sababu wachimbaji wanalalamikia Serikali kuchukua asilimia Hamsini (50%) ya uzalishaji.
Tunapenda kukanusha jambo hili la upotoshaji lenye nia ovu ya kuichafua Serikali na kutoa onyo kwa wale wote wanaofanya opotoshaji huo na hatua kali za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Vurugu zilizotokea kwenye mgodi huo ni kutokana na kutokubaliana mgawanyo wa hisa baina ya Wakurugenzi wa mgodi na Wamiliki wa Maduara.
TAARIFA HII IMETOLEWA NA OFISI YA AFISA MADINI MKAZI, MBOGWE.