Vurugu zaibuka Uganda baada ya Bobi Wine kukamatwa

Vurugu zaibuka Uganda baada ya Bobi Wine kukamatwa

Shing Yui

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
15,168
Reaction score
38,049
Ghasia zimezuka katika miji mbalimbali ya Uganda kufuatia kukamatwa kwa mgombea urais Robert Kyagulanyi.

Picha za angalau watu watatu wanaoaminika kuuawa katika ghasia hizo mjini Kampala pekee zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii huku mwanasiasa huyo akiendelea kushikiliwa katika korokoro ya polisi mjini Jinja ambayo imezingirwa na majeshi na polisi.

Milio ya risasi na mabomu ya gesi ya kutoa machozi ndiyo imehanikiza alasiri ya leo mjini Kampala wakati polisi walipokabiliana na waandamanaji wakidai kuachiwa kwa mgombea urais Robert Kyagulanyi.

Shughuli zimesimama katika mji wa Kampala wakati waandamanaji walipowasha moto katikati mwa barabara na katika ghasia hizo watu kadhaa wamejeruhiwa. Taarifa ambazo hazijathibitishwa rasmi zinasema kuwa angalau watu watatu wameuawa.

Kumeshuhudiwa michirizi ya damu iliyotapakaa kwenye barabara kuu ya Kampala.

Ghasia zimeripotiwa kutokea katika miji mingine ikiwemo Jinja ambako mwanasiasa Bobi Wine anaelezwa kuzuiliwa katika korokoro ya Nalufenya.

Kanuni za COVID-19 ndiyo chanzo​

Kukamatwa kwa Bobi Wine kunatokea siku moja tu baada ya mkuu wa jeshi la polisi kuwaonya makamanda wa jeshi hilo kuwa watawajibika na kuadhibiwa ikiwa wataruhusu wagombea kukiuka kanuni za kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19.

Hata hivyo, wanasiasa wa upinzani wanasisitiza kuwa kanuni za kudhibiti COVID-19 zinatumiwa tu kama kisingizio cha kuwakandamiza.
Hata hivyo kuna baadhi ya wanasiasa wa upinzani ambao wanawakosoa wenzao kwa kukaidi mwongozo waliopewa katika kuendesha kampeni hizo.

Kulingana na kanuni hizo mgombea haruhurusiwi kuwa na mkutano wa zaidi ya watu 200 na wote lazima wavalie barakoa.
Hadi wakati wa kutuma wa kuandaa taarifa hii polisi na wanajeshi walikuwa wameshika doria kali katikati ya mji na watu wengi wameshuhudiwa wakitafuta namna ya kurudi makwao.

1605723279654.png

Waandamanaji wameibuka #Kampala nchini #Uganda baada ya polisi kukamata mgombea urais Bobi Wine akiwa anaendelea na kampeni

Watu kadhaa wamefariki na wengine kujeruhiwa baada ya polisi jiji Kampala kujaribu kuzuia maandamano hayo kwa risasi za moto na mabomu ya machozi

Waandamanaji waliziba njia na kuchoma matairi mara baada ya kupata taarifa za kukamatwa kwa Bobi Wine, waandamanaji wengine walinekana wakichana picha ya Yoweri Museveni
 
Alikuja kupewa "SOMO" kwa swaiba wake dodoma.

Kama walivyo kwa waswahili wa Pemba, madikteta nao wanajuana kwa vilemba:

Tuyagalaa presidaaa gwenooo
 
Najua kuna Forum ya East Africa ambayo inachakanua yanayojiri kwa jirani zetu. Ila hoja yangu ya kuileta hii hapa ni kutokana kufanana sana hali yao na hali ambayo tungeweza kupitia, au karibu tupitie. Pili Forum hizo mara nyingi ni za Kiingereza na baadhi ya wanao 'dare to talk openly' hawawezi kufanya hivyo huko.

Jamani, kweli Tanzania tumebarikiwa kwa kupewa hekima. Wengine watasema ni upumbavu wetu. Au ni ushupavu wa vyombo vyetu vya usalama na 'ubwege' wa vyao? Haya nawaachia nyie, kwani miye sina meno ya kutafunia mbuyu!
 
Haya maelezo ndiyo ya Uganda kutokota? Eleza ni kwa namna gani Uganda inatokota.
 
Back
Top Bottom