Vurugu zazuka nje ya ukumbi wa uchaguzi Bawacha, Wafuasi wa Lissu na Mbowe wazichapa

Wakuu

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, ugomvi wa ngumi umezuka nje ya Ukumbi wa Ubungo Plaza unapofanyika mkutano wa uchaguzi wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha).

Ugomvi huo ulikuwa kati ya wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu dhidi ya wafuasi wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Soma, Pia: Uzi maalumu wa matokeo Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na Baraza la Wazee (BAZECHA) na wanawake (BAWACHA) CHADEMA Taifa 2025

Ingawa mkutano huo wa uchaguzi ulioanza mchana wa jana Alhamisi, Januari 16, 2025 unaofanyika ni wa wanawake, lakini waliorushiana ngumi walikuwa wanaume.

Chimbuko la ugomvi huo ni mabishano ya kuimarishwa kwa ulinzi, yaliyosababisha kutiliwa shaka mmoja wa watu waliokuwepo katika lango kuu la Ukumbi wa Ubungo Plaza.

Mabishano hayo, yalisababisha walinzi kuanza kumuondoa mtu huyo na wengine waliokuwepo eneo hilo na kuanzia hapo watu walianza kushambuliana.
View attachment 3204029
PICHA: Mwananchi

Pia, Soma:

-
VIDEO: Mbowe, Lissu wasalimiana kibabe BAWACHA, huku wakicheza kwa bashasha wimbo wa "Tuvushe Mbowe Tuvusheee"

-
Video: BAWACHA wamuunga mkono Tundu Lissu hadharani, wasema "Mabadiliko lazima"
Chama chawala kazini
 
Video ya tukio huna????
 
Back
Top Bottom