Vuvuzela zipigwe marufuku Tanzania

Nakubaliana na wewe
 
Mute
 
Waarabu wao ni mangoma na filimbi ushangiliaji wao.

Wazungu wao wanaimba nyimbo za timu yao.

Hii Vuvuzela kwalweli tutafute njia nyingine hata mimi inanikera balaa
 
Sikia bundesiliga wakipiga ngoma
Sikia epl wakiimba
Sikia la liga, seria a, league one wakipiga makofi

Njoo sasa tz mara kelele mara mianga ya kuumiza wachezaji
 
Mi zimeniathiri kisaikolojia nikiskia mpira mtangazaji anatangaza namsikia kama taarifa ya habari pamoja na makofi na filimbi ya refa naona hapo hamna kipute! Ila nikiingia nkaskia poooooooh kelele za kutosha mpaka Mzinga simsikii vizuri naona aah hapa leo ndo leo😅😅
 
Mlioanza kushabikia mpira juzi mna shida,simba na kikundi chao cha ushangiliaji 'kidedea' nilikuta wakipuliza tarumbeta 1988 nilipoanza fuatlia mpira
Dunia imebdilika. Vitarumbeta vile vya 1988 vilikuwa vinapulizwa pale shamba la bibi ambako ni wazi to kwa hiyo sauti zilikuwa zinsambaa hewani, hali siyo hivyo pale Lupaso kwani kelele zote zinaishia humo humo ndani.

Zaidi ni kwamba pitch ya vuvuzela ni ya juu sana kuliko trumpet au trombone; hivyo unaweza kukuta washangiliaji wakitumia trombone kwenye m[pira wa FIFA lakini vuvuzela ni marufuku.
 
Dah umenichekesha sana aisee na ukanikumbusha jambo kwenye mechi ya juzi ya Kagera vs Yanga. Ile mechi kuna muda mtalamu wa sauti upande wa Azam tv waliminya sauti za mashabiki, akawa anasikika mtangazaji tu. Basi Yanga walipopata goli la pili aliachia zile kelele kwa muda mwingi wa mchezo nikapata feeling fulani kuwa mechi imechangamka sasa na kasi imeongezeka kumbe ni yake makele ya uwanjani mtazamaji unaweza kuhisi mechi imechangamka au kupooza.
 
Coastal union huwa wanaspika kubwa uwanja mzima kelele tupu vuvuzela cha mtoto!!

Vuvuzela zinakera sana zinaanzia mitaani mchana siku za mechi ni fujo tupu.

Dizaini waafrika tuna utamaduni wa kupiga makelele kuanzia nyumbani wazazi wanafokea watoto kwa sauti kubwa mtaa mzima unasikia, nazo sub woofer chumba kimoja cha kupanga cha Gen Z nyumba nzima mnasikilizishwa singeli kwa nguvu mtake msitake!! Ni kero haswa!!

Ukipita kariakoo hakuna mahali pa kupiga cm ni kelele za matangazo kila kibanda ni kero kubwa haswa!! Mamlaka zindoe hizo spika inaitwa Noise pollution!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…