Vyakula 7 vitakavyomfanya mtoto wako awe na akili zaidi

Vyakula 7 vitakavyomfanya mtoto wako awe na akili zaidi

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
VYAKULA 7 VITAKAVYOMFANYA MTOTO WAKO AWE NA AKILI ZAIDI

Umuhimu wa lishe bora kwa mtoto sio katika kujenga mwili tu bali na afya bora ya akili. Mtoto mwenye afya bora ya akili ni mchangamfu na anaelewa mambo mbalimbali kwa urahisi.

Kwanza ni vizuri zaidi kumnyonyesha mtoto miezi sita ya kwanza bila kumpa chakula chochote ili awe na afya bora ya akili. Lakini pia uwepo wa vyakula tulivyotaja hapo chini kwenye milo ya mtoto wako kutamsaidia kuweza kufikia uwezo wake wa juu kiakili. Vyakula hivyo ni:
  • Mayai
  • Mtindi
  • Mboga za kijani
  • Samaki
  • Mbegu za mafuta na mafuta mazuri.
Mfano Karanga, Amonds, Mafuta ya Olive, Mafuta ya Alizeti n.k
  • Oats
  • Parachichi
Ubongo wa mtoto wako hukua kwa kasi sana katika miaka yake mitatu ya kwanza na ni kipindi muhimu zaidi kuhakikisha hakosi vyakula hivi kwenye milo yake.

👉Usikazanie kumpatia mwanao vyakula vya kumuongezea mwli tu vinaweza kumletea madhara mbeleni ya kiafya na kiakili pia
 
VYAKULA 7 VITAKAVYOMFANYA MTOTO WAKO AWE NA AKILI ZAIDI

Umuhimu wa lishe bora kwa mtoto sio katika kujenga mwili tu bali na afya bora ya akili. Mtoto mwenye afya bora ya akili ni mchangamfu na anaelewa mambo mbalimbali kwa urahisi.

Kwanza ni vizuri zaidi kumnyonyesha mtoto miezi sita ya kwanza bila kumpa chakula chochote ili awe na afya bora ya akili. Lakini pia uwepo wa vyakula tulivyotaja hapo chini kwenye milo ya mtoto wako kutamsaidia kuweza kufikia uwezo wake wa juu kiakili. Vyakula hivyo ni:
  • Mayai
  • Mtindi
  • Mboga za kijani
  • Samaki
  • Mbegu za mafuta na mafuta mazuri.
Mfano Karanga, Amonds, Mafuta ya Olive, Mafuta ya Alizeti n.k
  • Oats
  • Parachichi
Ubongo wa mtoto wako hukua kwa kasi sana katika miaka yake mitatu ya kwanza na ni kipindi muhimu zaidi kuhakikisha hakosi vyakula hivi kwenye milo yake.

[emoji117]Usikazanie kumpatia mwanao vyakula vya kumuongezea mwli tu vinaweza kumletea madhara mbeleni ya kiafya na kiakili pia
Mayayi yawe ya kienyeji
Ndizi mbivu na za kupikwa zisikosekane
 
Mayayi yawe ya kienyeji
Ndizi mbivu na za kupikwa zisikosekane
Mwanangu nilikuwa namnunulia ndizi mbivu anakula asubuhi na jioni kwa muda mrefu sana.

Sasa hivi kuna ishara naziona kwamba dogo anaenda kuwa mtu smart sana
 
Ndizi mbivu,mboga za majani na mayai ya kienyeji!hapa mtoto lazima awe poa sana aisee.
 
Yes mafuta ya samaki na dagaa yana content inaitwa Omega3 inasaidia sana kuimarisha afya ya ubongo.
Vipi dagaa wabichi tukiwakaanga na mtoto akala ina shida ama ale wakuchesmhwa ?
 
Back
Top Bottom