Honey Faith
JF-Expert Member
- Aug 21, 2013
- 15,782
- 11,819
Naomba nikumbushe kesho ila mimi nilikua nakula snickers
Ok sawa nitakukumbusha ila hata snickers napenda ila sio kivileee
Kumbe zabibu inasaidiakuongeza akili ? asante Mzizi kwa kunifundisha maana siku nyingi nilikuwa najiuliza mbona Mapandri wanaakili nyingi sana ? Leo nimepata jibu ni kwa sababu ya kunywa divai kila siku inayotengenezwa na zabibu
kahawa MziziMkavu naomba maelezo ya kina zaidi maana nasikia ina nicotine nyingi sana
vyakula ulivyotanja hapo nakubaliana navyo ispokuwa kahawa tu
Mkuu, kahawa na chocolate mimi hapana sababu ya caffeina iliyomo humo.
Tupe maelezo mazuri juu ya kahawa maana nasikia sio nzuri kiafya.
Mkuu Karanga ziwe mbichi itakuwa ni bora zaidi.Mkuu karanga mbichi au?
COFFEE (KAHAWA) Kahawa si kinywaji cha mtu kupendasana kutumia, lakini kinapotumiwa kwa kiasi kidogo na kwa tahadhari, kina faida zake:Kuhusu karanga/korosho nakubaliana na MziziMkavu kwa sababu kuna kitu inaitwa almond nayo inasifika kwa kuboresha ubongo.
Mananasi nayo niliona mahali yanasaidia uwezo wa kukumbuka.
Kuhusu kahawa........itabidi nikapitie upya hadidu rejea
Mkuu Karanga ziwe mbichi itakuwa ni bora zaidi.
COFFEE (KAHAWA) Kahawa si kinywaji cha mtu kupendasana kutumia, lakini kinapotumiwa kwa kiasi kidogo na kwa tahadhari, kina faida zake:
Huboresha utendaji kazi wa ubongo
Hutoa ahueni kwa wagonjwa wa asma (asthma)
Hutoa ahueni kwa wenye homa
Huongeza nishati ya mwili
Huzuia meno kuoza
Ina kemikali ambayo huzuia saratani kwa wanyama
Hutoa uchangamfu
Chanzo.MziziMkavu Hauchimbwi Dawa
COFFEE (KAHAWA) Kahawa si kinywaji cha mtu kupenda sana kutumia, lakini kinapotumiwa kwa kiasi kidogo na kwa tahadhari, kina faida zake:
Huboresha utendaji kazi wa ubongo
Hutoa ahueni kwa wagonjwa wa asma (asthma)
Hutoa ahueni kwa wenye homa
Huongeza nishati ya mwili
Huzuia meno kuoza
Ina kemikali ambayo huzuia saratani kwa wanyama
Hutoa uchangamfu
Chanzo.MziziMkavu Hauchimbwi Dawa
Vyakula 7 vyenye Faida kwa Ubongo na Akili yako!
Zabibu:
Husaidia kulinda ubongo dhidi ya kupungua uwezo wa kumbukumbu.
Samaki
Husaidia kuongeza uwezo wa Ubongo katika mawasiliano.
Kahawa:
Hulinda Ubongo dhidi ya ugonjwa wa Akili unao ambatana na uzee.
Chokleti (Chocolate):
Husaidia kulinda ubongo dhidi ya kupungua uwezo wa kumbukumbu.
Mtindi (Maziwa Mgando):
Huongeza Vitamini B12, ambayo husaidia kuzuia Ubongo Kusinyaa.
Mboga za Kijani / Majani:
Husaidia kulinda ubongo dhidi ya kupungua uwezo wa kukumbuka mambo.
Karanga au Korosho:
Huongeza Vitamini E, ambayo hulinda Ubongo dhidi ya ugonjwa wa Akili unao ambatana na uzee.
Karanga ndio ulevi wangu.