Pole sana.
Tatizo la acid reflux (GERD) na tumbo kujaa gesi huwa na visababishi vingi mfano ukiwa na maambukizi ya aina fulani ya bacteria wajulikanao kama H-pylori. Pia aina ya vyakula na mtindo wa ulaji huweza kuchangia hiyo hali kutokea.
Kwa hiyo ukiwa na tatizo hilo ni muhimu kwanza kwenda hospitali ili ukafanyiwe vipimo vya choo ili kama huyo mdudu, H-pylori ataonekana basi upatiwe dawa za kumuua.
Kama vipimo vipo kawaida basi ni muhimu kuepuka au kupunguza kula aina fulani ya vyakula ambavyo husababisha tatizo hilo kutokea baada ya kuvitumia. Hapa ni vigumu kutaja moja kwa moja vyakula vya kuepuka kwa sababu mara nyingi kila mtu kuna vyakula akila hupata/huchochea hiyo hali ya acid reflux (GERD). Kwa hiyo epuka au punguza kula vile vyakula ambavyo wewe mwenyewe unaona kuwa vinachochea hiyo hali ya acid reflux (GERD) kukupata.
Pia epuka kupanda kitandani/kulala muda mfupi baada ya kula. Inashauriwa ulale/upande kitandani walau saa 1 hadi 2 baada ya kula. Mara baada ya kula utumbo huzalisha acid nyingi kwa ajili ya kumeng'enya chakula kwa hiyo kulala mara baada ya kula husababisha acid reflux na hivyo kusababisha vichomi na kiungulia. Kukaa saa 1 hadi 2 baada ya kula huruhusu chakula kumeng'enywa na hivyo kupunguza tatizo la acid reflux.
Kama utafanya vyote hapo juu lakini bado hupati nafuu basi unaweza kwenda hospital kubwa wanapofanya vipimo vingine vikubwa vya kuchunguza mfumo wa chakula mfano OGD ili kubaini matatizo mengine yanayoweza kusababisha hiyo hali ya acid reflux (GERD).
Kila la kheri.