VYAKULA NA MAGONJWA: Hadhari kwa watumiaji wa samaki, chipsi

VYAKULA NA MAGONJWA: Hadhari kwa watumiaji wa samaki, chipsi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
attachment.php


KWA UFUPI


  • Jambo hili linafanywa sehemu mbalimbali kama vile nyumbani, migahawani, hotelini, shuleni na zaidi mitaani kwa wakaanga shipsi, mihogo, mandazi, samaki na kitimoto


Kama moja ya njia ya kupunguza gharama za matumizi, watu wengi wanatumia mafuta yaleyale zaidi ya mara moja kukaangia vyakula mbalimbali.

Jambo hili linafanywa sehemu mbalimbali kama vile nyumbani, migahawani, hotelini, shuleni na zaidi mitaani kwa wakaanga shipsi, mihogo, mandazi, samaki na kitimoto.

Watu wanaotumia mafuta zaidi ya mara moja inawezekana wanafuata mazoea na kijamii lakini kwa kujua ama kutojua hatari za hulka hiyo kiafya.

Mtu anavyotumia mafuta zaidi ya mara moja, ubora wa mafuta hayo unapungua. Mafuta yenye ubora mdogo yakitumika kukaangia vyakula yananyonywa mengi katika vyakula.

Mtu akila vyakula hivyo atapata uzito kupita kiasi, lehemu kwa wingi na shinikizo la damu. Vitu ambavyo vyote vinachochea ugonjwa wa kisukari na magonjwa ya moyo. Zaidi ya hayo, mafuta yaliyotumika kukaangia vyakula huwa yana mabaki ya vyakula. Mafuta hayo yakipoa vijidudu vya bakteria watakula mabaki hayo na kuzaliana kwa wingi.

Mafuta yenye mabaki ya vyakula yanapokosa hewa huwa yanaweza kuwa na mazingira mazuri ya bakteria aina ya "Clostridium botulinum" kuzaliana.

Bakteria wa aina hiyo anasababisha ugonjwa hatari unaotokana na ulaji wa vyakula vyenye sumu unaoitwa "botulism".

Kuyahifadhi mafuta katika friji au friza unapunguza bakteria kuzaliana. Lakini watu wa namna hiyo kwenye jamii huwa wanayahifadhi tena wakati mwingine kwenye mazingira machafu.

Mtu anavyotumia mafuta kukaanga vyakula zaidi ya mara moja, uwezo wa mafuta hayo kuhimili joto unapungua na yanaweza kuzalisha kemikali kama vile zinazoitwa "freeradicals" ambazo zinaweza kuharibu ubora wa chakula na

kuharibu chembehai na kuongeza uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa saratani. Mafuta yanayotokana na mimea yanahimili zaidi joto wakati wa kukaanga vyakula kuliko yale yanayotokana na wanyama.

Mafuta yaliyosafishwa pia, yanahimili zaidi joto kuliko yale yasiyosafishwa. Mafuta ya aina hiyo ndiyo yatumike.

Mafuta yaliyosafishwa ya zaituni (olive), jamii ya karanga, soya na alizeti ni miongoni mwa yale yenye uwezo mkubwa wa kuhimili joto kali na hivyo ni mazuri kwa matumizi ya kukaangia vyakula.

Kwa usalama wa afya na ubora wa vyakula vitakavyo kaangwa, watu wanashauriwa kutumia mafuta mapya kila wakati wanapokaanga vyakula. Hata hivyo, uzoefu unatuonyesha kuwa kwa watu wanaokaanga kiasi kikubwa cha vyakula ndani

ya chombo chenye mafuta mengi, siyo rahisi kila wakati kutumia mafuta mapya kwani ni gharama na inaweza kusababisha hasara.
Mafuta yanaweza kutumika zaidi ya mara moja kukaangia kwa masharti yafuatayo. Mtu anapokaanga vyakula asitumie moto mkali sana kwa sababu utaharibu mafuta na chakula anachokiandaa.

Hii haina maana kuwa atumie moto mdogo kiasi ambacho chakula hakitaiva na kushindwa kuua vijijidudu vilivyomo katika vyakula vibichi.

Mtu asichanganye mafuta mapya na yale yaliyotumika. Vyakula visiwekwe chumvi nyingi ili kulinda nguvu ya mafuta kuhimili moto.

Mafuta yakipoa, yachujwe haraka kwa kutumia kitambaa safi ili kuondoa mabaki ya vyakula. Mafuta yafunikwe na kuhifadhiwa katika chombo safi. chanzo.VYAKULA NA MAGONJWA: Hadhari kwa watumiaji wa samaki, chipsi - mwanzo - mwananchi.co.tz




 

Attachments

  • samaki.jpg
    samaki.jpg
    10.5 KB · Views: 731
Sehemu kubwa ya jamii ya watanzania hawana elimu ya lishe na wengine hawataki hata kufuatilia elimu ya lishe na namna bora ya ulaji kwa ujumla.Baadhi ni wabishi sana.Mfano swala la ulaji wa ugali wa Sembe ni tatizo sugu ktk jamii yetu.Naamini kama mabadiliko yatakuwepo labda itakuwa kwa kizazi kijacho na sio hiki.Kupendelea kula vyakula vya chap chap (fast food) kama chips na vyakula vingine vya kutosa kwenye mafuta ni hatari kwa afya ya walaji.USHAURI: elimu itolewe zaidi kwa wanawake kwani ndio walioshikilia gurudumu la maandalizi ya chakula.hayo ni maoni yangu.
 
Mmmmh !mkuu nimewaza kama hali ni hii basi nimekula sana hao bacteria maana home baada ya kukaanga mafuta huwa yanawekwa tuu kwenye chupa yake na kukaa jikoni loh! tayari kwa kukaanga kitu kingine
Na chipsi samaki nnazokula ofisini mmh! mbona kazi ipo
 
Back
Top Bottom