Vyakula sokoni bei iko chini sana

Kama kuna sehemu nimelaumu niko tayari kuomba radhi kwa watanzania mheshimiwa .
Ila nimerudia kusoma aya kwa aya,neno kwa neno andiko langu limegubikwa na furaha na tabasamu kwa bei kuwa chini
Nitoe wito na wewe kurudia kusoma

Mama oyeeee
 
MAMA ANAENDELEA KUUPIGA MWINGI. KONGOLE KWAKE
 
Hata wakulima wa mpunga gunia bado ni sh 60 elfu kilimo hakieleweki
Mpunga mwaka huu umegoma kupanda ndio maana mchele uko chini,hiyo bei ya 60 ni wapi huko
 
Soko Ilala,kisewe vitu Bei chee sanaaa..

Nilienda mwanza sikula SAMAKI Bei juu Sanaa bora kununua NYAMA Kama una familia hapo mwanza mzunguko wa pesa ni mdogo Sana.

Ila dar es salaam SAMAKI, KUKU Bei chee kilo 12,000 Ila mwanza pesa ni ngumu Sana na maisha yapo juu Sanaa

Dar pesa ipo nje nje Sanaa 😊 Ibarikiwe DAR ES SALAAM ☺️
 
Kuna umuhimu wa watu kutembelea masoko badala ya kulia bei huku wanaonunua kwenye masoko kama mnazi mmoja na kule Masalia au mbezi mwisho kwa mabepari

USSR
Mbezi Mwisho zile bei ni uhujumu uchumi wa wakazi wa maeneo yale.
Kule vingine vinazidi bei ya Mbezi Beach.
 
Mvua nyingi za msimu uliopita mazao mengi yamekutana sokoni.
Subiri miezi michache utarudi kulia bei kubwa hapa hapa.
Sasa kilio kwa wakulima.
Pilipili mwendokasi ndoo kubwa nimetoka kuuza 30,000 bei ya jumla sasa nimeuza 7000.
Nimeziacha zioze shambani.
 
Niliambiwa na mzee mmoja kiwa soko la Buguruni na temeke ndio masoko yenye bidhaa zenye bei ndogo zaidi kwa Dar nzima,hii ni kutokana na jamii iliyomzunguka masoko hayo ni ya kimaskini hata karoti na hoho wanauza hadi nusu kwa hamsini

USSR
soko la temeke unamaanisha TANDIKA au stereo?
Uko sahihi,soko la temeke ndio funga kazi,vitu bei chee sana
Soko la temeke ndo lipi tandika au stereo?
asee siku nmeenda mwanza nikikasirika. yan nlikua nasikia wanavosifia ooooh mwanza jiji la samaki na sato. mweeee sku nmeenda mwanza, ile kuulizia samak wa kukaangwa tena wa size ya kawaida tu eti wananambia elf 3. wakat samak huyo huyo dar nauziwa 1500.
Mbezi Mwisho zile bei ni uhujumu uchumi wa wakazi wa maeneo yale.
Kule vingine vinazidi bei ya Mbezi Beach.
mbez mwisho nako kuna maisha ya ajabu sana. sku moja nlikua natafuta unga wa mtama, sasa kwenda dukan naulizia wananambia kilo ya mtama ambao haujasagwa bei ni elf 3. nkaacha nkaenda bugurun nkakuta kilo ya unga wa mtama( yaan tayar ushasagwa) bei ni 1500 asee nlishangaa sana.

ila nlichogundua n kwamba, maeneo yenye wachaga wengi maisha huwa yanakua magumu sana by nature hata kimara napo pana maisha ya kiwaki sana. nmeishi moshi pia nako maisha magumu balaa.
 
Buguruni inauzwa mpaka hoho nusu, yaani unaenda unakatiwa hoho nusu unaenda kuunga mboga
Kabisa huo ndio ukweli hata nusu nyanya na nusu kitunguu ikumbukwe Buguruni ndio walianzisha kuuza utumbo, kichwa na miguu ya kuku bila kusahau ngongingo aka mkia wa kuku

USSR
 
Wachagga wanapenda faida bila sababu ya msingi ,soko la mbezi mwisho ni soko la hovyo kuliko yote duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…