Vyakula vipi vinaleta wateja?

Mimi mstaarabu

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2020
Posts
262
Reaction score
577
Ukiwa unataka kufungua restaurant au mgahawa. Unatakiwa uwe na ujuzi wa vyakula vya aina gani?

Vile vile ni vyakula vipi ni pendea sana na vinaleta wateja?
 
Mbagala Dar
 
Dah.. umenena vyema...
Ongezea:
1. Supu ya pweza
2. Urojo
3. Al-kasusu
 
Mbagala Dar
Kwa Mbagala ndugu yangu jitahidi yafuatayo

Asubuhi:
Chai, Chapati, Maharage (yale wanaweka sukari), supu ya utumbo mihogo na vidagaa vile vya mchele

Mchana: Ugali na wali... vitafunwa visikosekane maharage, mchicha, samaki(vibua)/dagaa, bamia.

.jioni
wakati unaandaa ya usiku jitahidi uwe na supu ya pweza kiaina
.
Usiku
Ubwabwa na vitafunwa kama maharage, nyama na samaki. Usisahau pilipili na ndizi mbivu.

Kama mtaji unaruhusu weka kafriji kuwemo maji ya chupa na ya kienyeji, soda na mtindi

Ahsante kwa kunisoma na kunishukuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…