Vyakula vipi vinaleta wateja?

Vyakula vipi vinaleta wateja?

Mimi mstaarabu

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2020
Posts
262
Reaction score
577
Ukiwa unataka kufungua restaurant au mgahawa. Unatakiwa uwe na ujuzi wa vyakula vya aina gani?

Vile vile ni vyakula vipi ni pendea sana na vinaleta wateja?
 
Inategemea uko wapi...

Kama uko Iringa, hakikisha huchezi mbali na nyama ya wow wow wow!

Kama uko "Ntwala" hakikisha kile kitoweo pendwa cha nyau hakikosekani kwenye menu yako

Kama uko Moshi, usihangaike sana na msosi una ladha gani, we hakikisha tu chini ya meza una machupa kadhaa ya K Vant kwa ajili ya kupimia wateja vipimo vya kanywaji

Kama uko Mbeya, hakikisha kitimoto unafuga mwenyewe karibia na kiwe

Kama uko Dar, hakikisha huchezi mbali na vyepe, mayai na wahudumu warembo wasiojua kusema No...

Kama uko maeneo mapya ya ujenzi, ugali maharage na mtindi vitakutoa

Mengine ntakuambia uliniambia uko wapi...
Mbagala Dar
 
Dah.. umenena vyema...
Ongezea:
1. Supu ya pweza
2. Urojo
3. Al-kasusu
 
Mbagala Dar
Kwa Mbagala ndugu yangu jitahidi yafuatayo

Asubuhi:
Chai, Chapati, Maharage (yale wanaweka sukari), supu ya utumbo mihogo na vidagaa vile vya mchele

Mchana: Ugali na wali... vitafunwa visikosekane maharage, mchicha, samaki(vibua)/dagaa, bamia.

.jioni
wakati unaandaa ya usiku jitahidi uwe na supu ya pweza kiaina
.
Usiku
Ubwabwa na vitafunwa kama maharage, nyama na samaki. Usisahau pilipili na ndizi mbivu.

Kama mtaji unaruhusu weka kafriji kuwemo maji ya chupa na ya kienyeji, soda na mtindi

Ahsante kwa kunisoma na kunishukuru.
 
Back
Top Bottom