Vyakula vipi vinanenepesha mwili?

shalet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
3,430
Reaction score
3,547
Habarini wakuu,

mwanzo kabla ya 2013 nilikuwa na mwili wa kawaida badae nikaugua karibia miaka miwili sasa nipo kwenye recovery lakini mwili wangu bado umekondeana nashindwa kuelewa ni vyakula vipi nitumie manake najaribu kuongeza quantity ya msosi lakini wapi nimegoogle napewa mjina ya vyakula ambavyo ni vigumu kuvipata majina very strange.

Note: sitafuti kuwa mnene ila mwili fulani nionekane giant kidogo.
 
Mkate ongeza na blueband, viporo kama wali, vitu vyenye sukari kama soda kunywa bila kujinyima, vyakula vya ngano maandazi na chapati, ugali Wa bila kukobolewa, uji Wa lishe weka na maziwa na blueband, supu uwe unaongeza blueband na mtori yaani kama mzazi katoka kujifungua nakwambia usiponenepa uje tena nikuongezee misosi mingine. Na mboga zipikwe na Katanga wakati mwingine Nazi.
 
Kunenepa ni NATURE zaidi kuliko unavyofikiria ww! Hicho hicho unachokula www akila mwenye nature ya kunenepa unaona anafumuka anakuwa kifutu tena kwa muda mfupi sana
 
Nashukuru kwa ushauri huu nitaufuata.
 
Kila siku asubuhi saa nne na saa kumi jioni piga ugali wa dona au muhogo na kitimoto kilo mbili shushia bia nne uzipendazo kila ufanyapo hivi na kabla ya kulala hakikisha unamaliza bia tano kama hautoweza jifunze kusoma soma vitu kwenye internet au fanya kitu kitakacho kukeep busy ili uweze kunywa bia hizi 5 usiku. Ukiwa katika hali ya ubora itakuchukua wiki mbili au tatu kunenepa trust me. Nilipotoka mafunzo ya JKT nilipungua toka 93 mpaka 63 lakini ndani ya mwezi nilikuwa na kilo 103
 
Kwanzavkapime ngoma ujue ukondefu Ni kwasababu ya ugonjwa ama afya dhoofu kwasababu ya lishe. Cha pili achilia moyo maana kama una karoho ka korosho hata ungekula VIP hunenepi ,hivo ka moyo kasijikunje, tatu pendelea kula chips mayai ya kisasa, kuku wa kisasa, kitu moto kwa sana , kataa mawazo yalokuzidi umri, n.k
 
Kitimoto na bia, mwezi mmoja tu unakuwa kama marehemu komba.
 

Kula Proportional Complete Diet,
 
nashukuru kwa ushauri mkuu ila ngoma sina.
 
Unene ni shida watu wengi hawataki kusikia hii story.. Ushauri tu tafuta amani, furaha, na upende mazoezi. Hata ule mihogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…