Vyakula vya ajabu nilivyowahi kula

Nlikuwa bangalore masomoni, siku moja tumeenda study tour Goa, ni mji kama bagamoyo kwa huku. Ila ji mbali kama 1300km toka goa hadi bangalore. Tulivofika tukaingia kula. Mi nikaagiza fried rice ndo wali kidogo unafanana na wa kwetu ila mbaya balaa na kingfish, kuletewa nikawekewa na bakuli lingine pembeni, basi bwana ilikuwa usiku kwenye ka mwanga hafifu hivi saa nne za usiku mm nikamimina mchuzi wa samaki na filet ya samaki. Nikachukua na mchuzi mwingine nikamimina sasa wakati nakula namalizia nikawa nimemaliza nyama ya samaki, nikaenda kwenye lile bakuli dogo nile na kilichomo. Nlikutana na konokono wamejaaa. Nikatamani kujitapsha. Nikawamind balaa wenye hoteli. Pasi wakaomba msamha ila jamaa yangu kutoka malawi alikula konokono wale
 
Nakumbuka nlipiga hii picha
 

Attachments

  • 20210301_055405.jpg
    76.3 KB · Views: 38
Story yako inatufundisha nini ?
 
Kuna nikikumbuka nachekaga sana,,, miaka hiyo utotoni songea uko kuna mdau wetu mmja kwao walikua wapo kama wanne ivi wanaosoma sasa kuna siku wenzake wamewai kuludi toka shule wakala ugali mboga wakamaliza alaf ukabakia ugali tupu sasa muhuni kaludi kakuta ugali tupu yaani jamaa akapenga kamasi akala na ugali yan ukimkumbusha mbak leo jamaa anachukia kinoma Dadek
 
khaa sio kweli mkuu duuh
 
Aaah Mzee wa kibao. Ulienda tena kwa Mzee kupata kingine? Maisha haya yana mengi ya kujifunza ikiwemo na vyakula vya aina tofautitofauti
 
Nilikua member kwa Wachina ,siku nikakuta minyoo na vyura sikurudi tena mpk leo miaka 10.
 
Mlipata wapi chanzo cha moto wa kumchoma nyani huyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…