Vyakula vya ajabu nilivyowahi kula

Vyakula vya ajabu nilivyowahi kula

Kitoabu

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
10,677
Reaction score
11,768
"Hata Nguruwe huwa ana swih mbele ya njaa ya kufa"

Hii kauli niliwahi kumsikia Fid Q kwenye moja ya nyimbo zake, kitambo kidogo.

Muda huo nakula ugali wa kengele, yani dereva wa sahani break mkeka.

Nilipo kuwa nausikia mstari huu, kila siku nilikua najisea kua hata iwe vipi sintokuja kula nguruwe, sababu jamii yangu, dini yangu hairuhusu kula nguruwe.

Miaka mingi imepita, ule ugali wa kengele umeota mbawa, nasasa ni mwendo wa asie fanya kazi na asile, yani ni Jitegemee sio makongo tena.

Katika kujitafutia mwenyewe riziki ndipo sasa nakubaliana na msemo wa fid q " hata nguruwe huwa anaswih mbele ya njaa ya kufa" baada ya kukutana na nyakati ngumu za utafutaji riziki (hususan chakula)

Leo nataka niwashirikishe, ama niwahabarishe vyakula vya ajabu nilivyo wahi kula, ambavyo sikutegemea kama nitakuja kula kwenye maisha yangu.

1- PANYA
Ebwana eh, Mndengereko ukitaka akunyime maji basi atambue kua wewe ni mla panya.

Kwetu panya aliwi kabisaa tena ni kinyaa, lakini mimi nimekula.

Nakumbuka ilikua mwaka 2018, nikiwa nachimba poli la Nacoja (inasomeka nakocha)

Kulikua kuna nyumba moja hivi, ya bibi yangu wa kimakua, huyu alikua mganga, nilikua nikitoka Nanhupo (ninapo ishi) lazima nipite hapo kijijini (Nacoja) kwa huyu bibi, nioge dawa ndio niingie polini (mgodini)

Mazoe hayo yalipelekea pale nyumbani kwa yule bibi nichukuliwe kama mwana ndugu, kwani nilipo kua nafika hapo nyumbani lazima nibebe vijizawadi.

Siku moja, nimetoka zangu polini mida ya jioni, jua lishazama, nikaona kwa muda huu siwezi kupata piki piki ya Nanhupo, nikaamua kulala pale kijijini kwa yule bibi yangu.

Hii si mara yangu ya kwanza kulala hapa. Ni nyumba kubwa yenye wanafamilia wengi, pia kuna mtoto mmoja wapo wa yule bibi ni lika langu, hivyo huyu bibi alikua anani chukulia kama mwanae tu.

Niliingia pele, nikamkuta dada mkubwa yuko jikoni anaandaa ugali, nikamsalimia, nikaingia chumbani kubadili nguo za kazi.

Mara haukupita muda mrefu, nikaitwa kwa ajili ya kula. Sahani yetu ilikua ya watu kama wanne hivi, akiwemo yule mtoto wa kiume wa yule mama na watu walio nizidi umri kama wawili hivi.

Kabla ya kuanza kula yule mshikaji wangu, akaniuliza "unaaliya mavala?" akimaanisha kua ninakula panya, nikamjibu ndio.

Neno mavala mimi nikahisi kaniuliza kama nina kula mbawala, hivyo nikamjibu ndio. Nikawanawa maji na show ikaanza.

Matonge kama manne matano, mara, mmoja wa wale wazee akazama ndani ya bakuli nakutoa kitoeo na kukiweka kwenye sahani, amadi nakuta panya katula, mkia huo.

Kidogo nitapike lakini nikajikaza kisabuni, kwanza nijiuliza kama nitanawa maji, wenyeji wangu wangenichukulia vipi? tena ukizingatia walisha niuliza. Nikaona sio poa, na mimi nika kamata wakwangu nikaweka pembeni. Kwa kweli nilijilazimisha mpaka nikammaliza.

Miaka miwili sasa tangu tukio hilo kupita, cha ajabu nimekua nawapenda panya kufikia mpaka nawalipaga watoto waende wakanichimbie huko mapolini.

Panya ananoga ukimkaanga na Mafuta kisha ukapata kachumbari na pili pili nyingi, mbele yako upo ugali wa muhogo.

Kwa hapa Tete panya anauzwa kwenye sahani kama samaki wa kukaanga, haiwezi pita week bila kula panya. Kiufupi panya ni mtamu na najuta kuchelewa kumjua.

2- CHURA
Hii ilikua huko huko polini Nacoja, tafauti ni kua huku sio kijijini bali ni porini.

Polini kula vitu vya ajabu haishangazi lkn si wote wanaokula vitu vya hovyo.

Binafs nilikua nina kinyaa sana kula vitu vya hovyo lkn kubanwa na njaa usiombe.

Kuna nyakati ufanyaji wetu wa kazi hupitiaga nyakati ngumu sana , hasa kiangazi, tena zaidi ni kuanzia mwezi wa kumi, kumi na moja na mwanzoni mwa mwezi wa kumi na mbili.

Narudi muda si mrefu
 
we jamaa ukija kuwa babu wajukuu zako watakua wanakupenda mpaka utashangaa,likizo wote watang'ang'ania kwenda kwa babu,hebu fanya urudii uendelee.
 
1. "Kombucha tea"(fungus tea) nilishawahi kunywa sana ina kauchachu flani siku hizi haipatikani sana.

2. "Mbesi" samaki alieoza au kuchina analiwa sehemu za Ifakara

3."Dadii" pombe ya kienyeji ya sehemu za Arusha.Unakunywa unalewa na unashiba.
 
Duh pole sana dogo
Aisee mkuu umenikumbusha mbali kweli, kuna kipindi tulilala njaa nyumbani afu asubuhi pia hamna chakula. Njaa inauma hatari sana mm na dogo tukawaza twende shambani kwetu. Sasa kwetu ni mwiko kuchukua kitu cha kula bila kupewa na mzazi sasa tukaona hapa tukichuma mahindi twendenayo nyumbani itakua msala. Tulikaa shambani tukagonga mahindi mabichi hadi tumbo likajaa njaa ikapotea.

Mungu mkubwa hatukuumwa
 
Hahaha umenikumbisha kipindi Fulani nikiwa kwenye mgodi Chunya huko machimbo ndo naanza anza bado chalii hali ngumu halafu kuna chatu alijipitisha kanona balaa tukamuua tukatengeneza supu matata na minofu mingine tukachoma tulikula kama siku mbili hivi

Tokea hapo tukaanza kazi ya kuwinda chatu. Mpaka saivi aisee katika vitu namiss maporini no nyama ya chatu
 
"Hata Nguruwe huwa ana swih mbele ya njaa ya kufa"

Hii kauli niliwahi kumsikia Fid Q kwenye moja ya nyimbo zake, kitambo kidogo.

Muda huo nakula ugali wa kengele, yani dereva wa sahani break mkeka.

Nilipo kuwa nausikia mstari huu, kila siku nilikua najisea kua hata iwe vipi sintokuja kula nguruwe, sababu jamii yangu, dini yangu hairuhusu kula nguruwe.

Miaka mingi imepita, ule ugali wa kengele umeota mbawa, nasasa ni mwendo wa asie fanya kazi na asile, yani ni Jitegemee sio makongo tena.

Katika kujitafutia mwenyewe riziki ndipo sasa nakubaliana na msemo wa fid q " hata nguruwe huwa anaswih mbele ya njaa ya kufa" baada ya kukutana na nyakati ngumu za utafutaji riziki (hususan chakula)

Leo nataka niwashirikishe, ama niwahabarishe vyakula vya ajabu nilivyo wahi kula, ambavyo sikutegemea kama nitakuja kula kwenye maisha yangu.

1- PANYA
Ebwana eh, Mndengereko ukitaka akunyime maji basi atambue kua wewe ni mla panya.

Kwetu panya aliwi kabisaa tena ni kinyaa, lakini mimi nimekula.

Nakumbuka ilikua mwaka 2018, nikiwa nachimba poli la Nacoja (inasomeka nakocha)

Kulikua kuna nyumba moja hivi, ya bibi yangu wa kimakua, huyu alikua mganga, nilikua nikitoka Nanhupo (ninapo ishi) lazima nipite hapo kijijini (Nacoja) kwa huyu bibi, nioge dawa ndio niingie polini (mgodini)

Mazoe hayo yalipelekea pale nyumbani kwa yule bibi nichukuliwe kama mwana ndugu, kwani nilipo kua nafika hapo nyumbani lazima nibebe vijizawadi.

Siku moja, nimetoka zangu polini mida ya jioni, jua lishazama, nikaona kwa muda huu siwezi kupata piki piki ya Nanhupo, nikaamua kulala pale kijijini kwa yule bibi yangu.

Hii si mara yangu ya kwanza kulala hapa. Ni nyumba kubwa yenye wanafamilia wengi, pia kuna mtoto mmoja wapo wa yule bibi ni lika langu, hivyo huyu bibi alikua anani chukulia kama mwanae tu.

Niliingia pele, nikamkuta dada mkubwa yuko jikoni anaandaa ugali, nikamsalimia, nikaingia chumbani kubadili nguo za kazi.

Mara haukupita muda mrefu, nikaitwa kwa ajili ya kula. Sahani yetu ilikua ya watu kama wanne hivi, akiwemo yule mtoto wa kiume wa yule mama na watu walio nizidi umri kama wawili hivi.

Kabla ya kuanza kula yule mshikaji wangu, akaniuliza "unaaliya mavala?" akimaanisha kua ninakula panya, nikamjibu ndio.

Neno mavala mimi nikahisi kaniuliza kama nina kula mbawala, hivyo nikamjibu ndio. Nikawanawa maji na show ikaanza.

Matonge kama manne matano, mara, mmoja wa wale wazee akazama ndani ya bakuli nakutoa kitoeo na kukiweka kwenye sahani, amadi nakuta panya katula, mkia huo.

Kidogo nitapike lakini nikajikaza kisabuni, kwanza nijiuliza kama nitanawa maji, wenyeji wangu wangenichukulia vipi? tena ukizingatia walisha niuliza. Nikaona sio poa, na mimi nika kamata wakwangu nikaweka pembeni. Kwa kweli nilijilazimisha mpaka nikammaliza.

Miaka miwili sasa tangu tukio hilo kupita, cha ajabu nimekua nawapenda panya kufikia mpaka nawalipaga watoto waende wakanichimbie huko mapolini.

Panya ananoga ukimkaanga na Mafuta kisha ukapata kachumbari na pili pili nyingi, mbele yako upo ugali wa muhogo.

Kwa hapa Tete panya anauzwa kwenye sahani kama samaki wa kukaanga, haiwezi pita week bila kula panya. Kiufupi panya ni mtamu na najuta kuchelewa kumjua.

2- CHURA
Hii ilikua huko huko polini Nacoja, tafauti ni kua huku sio kijijini bali ni porini.

Polini kula vitu vya ajabu haishangazi lkn si wote wanaokula vitu vya hovyo.

Binafs nilikua nina kinyaa sana kula vitu vya hovyo lkn kubanwa na njaa usiombe.

Kuna nyakati ufanyaji wetu wa kazi hupitiaga nyakati ngumu sana , hasa kiangazi, tena zaidi ni kuanzia mwezi wa kumi, kumi na moja na mwanzoni mwa mwezi wa kumi na mbili.

Narudi muda si mrefu
Nyama ya Mamba
Hii ni tamu sana yani sawa na nyama ya kuku halafu ni white meat.
 
Hivi Kwanzaa kabla ya kushusha mistari Tanapa wanapita humu ?

Eeh bwana basi mi na wanangu wa manzese maisha yalitupiga dar wengine wakawa wanatafutwa kwa wizi tukaamua twende pori flani tuanze biashara ya kukamata nyani na kuwauza hii biashara hipo kwenye hicho kijiji halafu kuwashika ni simple tu kikubwa tulikuwa tunawaekea ugoro kwenye ndizi akielewa tunae

Basi bwana siku hiyo katika kukamata askari wanyamapori hao hapo tulikimbia kichizi mwenzangu mmoja alipigwa shaba ya mguu tulikuwa wanne watatu tukaendeleza mbio huku mwanangu mmoja akiwa amembeba nyani mgongoni tunakimbia ule msako ulikuwa mkubwa Sana ilitubidi tuishi kwenye pango kwa siku kadhaa tutulie maana tungetokea vijiji jiran tungeshikwa pia tungetokea ng'ambo nje ya msitu tungeshikwa

Sasa kibarua kinaanza hio sehemu ya pori tuliojificha imefunga Sana (closed canopy) kibaya vinyama vidogo huvioni hata matunda Hakuna mengine yalikuwa rangirangi tukaogopa kula pengine ya sumu basi tulimchuna Yule nyani tukamchoma tukala maana njaa ilizidi sasa

Daah na ile njaa ilitubidi tule nyani
 
[/QUOT
Nyani ana ladha gani mkuu!
Nataka Ni test Kuna manyani yananizingua Sana hapa shambani
 
Hahaha umenikumbisha kipindi Fulani nikiwa kwenye mgodi Chunya huko machimbo ndo naanza anza bado chalii hali ngumu halafu kuna chatu alijipitisha kanona balaa tukamuua tukatengeneza supu matata na minofu mingine tukachoma tulikula kama siku mbili hivi

Tokea hapo tukaanza kazi ya kuwinda chatu. Mpaka saivi aisee katika vitu namiss maporini no nyama ya chatu
Duh...
 
sisi japokuwa sio wenyeji wa kusini ila panya tumekula sana,tena si kwa matatizo ni utundu tu.

tukiwa tunachunga ng'ombe kwenye masizi ya majani yaliyochomwa kazi ilikuwa ni moja tu,kukagua mashimo ya panya,na kuingiza fito za mianzi(unachomeka kwa utulivu kupima kama kunabonyea basi ni yess,tunachimba kwa panga mpaka anatoka+moto fresh.

kobe ndio tulimla kwenye eneo la shida kidogo,tukiwa mafunzoni huko porini unakula ugali hata kilo nne hushibi,kuna makobe kibao,weekend moja mhuni mmoja akaja na idea ya kula kobe+tulimbeza ila baadae kobe wakaanza kuadimika,maana ukawa ndio utaratibu sasa.
 
kobe na konokono nimekula sana konokono wako kama firigisi ukiwa unakula
 
Back
Top Bottom