Vyama vingi vilikubalika ili kuwaonyesha mabeberu kuwa tuna utawala wenye demokrasia

Vyama vingi vilikubalika ili kuwaonyesha mabeberu kuwa tuna utawala wenye demokrasia

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Niliongea na jirani yangu ambae ni kada kindaki ndaki, aliniambia upinzani hauwezi kutangazwa mshindi hata ukishinda. Nilimuuliza ni kwanini iwe hivyo? Jibu lake ni kuwa CCM na watu wake walijitoa mhanga katika ukombozi wa bara la Afrika na wamewekeana kiapo na vyama vyote vilivyopugania uhuru kuwa wao wataendelea kutawala.

Maswali yangu mengine hayakuwa na majibu kutoka kwake. Mwisho tulibadilisha mjadala na kuhamia kwenye hali ya hewa, hapa tulikubaliana wote kuwa mvua inanyesha. Kumbe kukubali kwetu vyama vingi ilikua ni njia ya kuendelea kupata misaada kutoka kwa mabeberu.

Vyama vingi vimechangia chachu ya maendeleo katika nchi zilizoendelea. Ninawaza jinsi Conservatieve au Republican wajinasibu hadharani kuwa watashinda tena ushindi wa kishindo kwakua dola iko kwenye mamlaka yao. Kesho mngesijia riots na matairi kuchomwa barabarani.

Chama kinapokua upinzani inabidi kijipange kuelekea uchaguzi mkuu ( kama ni uchaguzi huru na wa haki). Katika mipango yao kwanza watamchagua mtu anaefaa kuongoza na anaeweza kuwaletea ushindi. Labour walikaa bench kwa miaka mingi mpaka miaka ya 90 walipowekeza nguvu kwenye damu changa na kumpata Tony the Blairwna Gordon Brown waliyoiletea lLabour ushindi mkubwa 1997. Democratic walimuona Obama anafaa na walipompa ridhaa aliweza kuindoa Republican madarakani.

Tuachane na utawala wa mazoea tukubali mabadiliko. Mbona tuliweza kuachana na simu za mezani na siku hizi karibu kila mtu ana mobile mfukoni au kwenye mkoba wake.
 
CCM inajipendekeza Sana kwa mabeberu.
_104172054_capture.jpg
 
Chadema inashindwa tena uchaguzi huu kama chaguzi zilizopita. Uchaguzi huu Chadema itaanguka zaidi kwa sababu ya kauli za kupinga maendeleo.
Inabidi Chadema wajipange vizuri kwa uchaguzi wa 2025. Waache kusingizia tume. Wajitathmini wao wenyewe.
 
Chadema inashindwa tena uchaguzi huu kama chaguzi zilizopita. Uchaguzi huu Chadema itaanguka zaidi kwa sababu ya kauli za kupinga maendeleo.
Inabidi Chadema wajipange vizuri kwa uchaguzi wa 2025. Waache kusingizia tume. Wajitathmini wao wenyewe.
Tusubiri 28/10 maana huku kitaa Lissu anaeleweka asikwambie mtu. Hahitaji wanajeshi wakiovaa sare za chama, malori wala wasanii kujaza uwanja.
 
Back
Top Bottom