Vyama vya siasa feki Tanzania

MWFK, Msanii, na wengine...

Chama Cha Mapinduzi nakichukia kuzidi shetani mwenyewe.

Lakini naomba kuuliza hili: mnadhani ni chama gani kinaweza kuleta mabadiliko?
 

Ha ha ha ...wewe kama kawaida yako na upeo wako unaishia kwa
 

Jamaa waliamua tu kudeal na EPA peke yake na kuacha wizi mwingine wote wa BOT. Na hata hiyo EPA ambayo waliichagua, bado hawajakagua wizi wote (waliamua kuchunguza mil 133 kati mil 254 in question) na hata hapo bado wameshindwa kutoa report za nini walipata na wamefanya nini.

ndio maana bado nashikilia kuwa ufisadi ni sera ya ccm na wale ambao wako radhi na status quo ni mafisadi tu kama kina Mramba, Mgonja na wenzao.
 
Mwafrika wa kike,mimi huwa sipendi unafiki na unazi wa kijinga.Penye kusifia nitasifia hata kama simpendi ninayemsifia na Penye kukosoa nitakosoa hata kama nampenda ninayemkosoa.
Wewe kama unayaona hayo maoni yangu ni ya kifisadi ni hiyari yako na sikulazimishi uyakubali.Lakini ukweli ni kuwa watanzania walio wengi hasa wa vijijini bado wana imani na ccm kuliko upinzani.Kwanini?nikisema mimi utaniita fisadi,labda ukipata muda ujaribu mwenyewe kufuatilia hili.Sasa wakitokea watu wa kuyasema haya kwa faida ya upinzani ili wapange mikakati mizuri ya kwenda kuchukua kura nyingi kule vijijini,wewe unawaita mafisadi.



Ufisadi ni sera ya ccm kama ulikuwa hujui.

Unaweza kunionyesha mahali kwenye katiba au ilani ya ccm panaposema kuwa sera ya ccm ni ufisadi?



Hicho chama unataka kipatikane toka mbinguni?

Chama hakiwezi kutoka mbinguni hata siku moja.Chama lazima kitoke tanzania na kitengenezwe na watanzania.Kitapatikana,mimi bado nina imani hiyo.Lakini kwa sasa bado hakipo.



Huwezi kuleta hoja ambayo haina majibu hapa kwa sababu hii sio wonderland. Huwezi kusema ccm ni fisadi bila kutoa alternative. huwezi kukosa chaguo maana at the end of the day lazima kuwe na chama kinachoongoza.

kwako inaonekana chama chenye website nzuri lakini kikiiba mabilioni ya nchi na kuuza nchi kwa wageni huku wanawake na watoto wachanga wakifa kwa magonjwa yanayotibika ni bora kuliko chama ambacho bado kinajenga website yake.[/QUOTE]


Sasa kama hiyo altarnative haipo nitailazimishaje?maanake mimi bado sijaiona hiyo alternative unayoing'ang'aniza hapa.
Mimi sizumgumzii uzuri wa website ya chama.Nazungumzia umakini wa chama.Na umakini unaweza kuonekana hata katika vitu vidogo kabisa.Kwa mfano ile website ya richmond aliyotuonyesha siku zile Mwakyembe.Yaani ukiangalia ilivyo tu unagundua kabisa hawa watu wana walakini.Sasa unaweza kulinganisha na ule mfano mwingine hapa.
 
MWFK, Msanii, na wengine...

Chama Cha Mapinduzi nakichukia kuzidi shetani mwenyewe.

Lakini naomba kuuliza hili: mnadhani ni chama gani kinaweza kuleta mabadiliko?

ABC.... Any-party But CCM.

Unajua hapa Marekani, watu wengi hawategemei kuwa Democrats ni tough enough kwenye masuala ya security. Lakini ukiangalia exit polls za uchaguzi wa mwaka 2006, wananchi walisema anything but republicans na democrats wakachukua house na senate.

Kuna wakati ambapo chama kinakaa kwenye uongozi muda mrefu na kinadhani kuwa kinaweza kufanya chochote kile. Kwa sasa kwangu mimi any-party but ccm ni sera yangu.
 
Mwafrika wa kike,mimi huwa sipendi unafiki na unazi wa kijinga.Penye kusifia nitasifia hata kama simpendi ninayemsifia na Penye kukosoa nitakosoa hata kama nampenda ninayemkosoa.

Una hakika kuwa hupendi unafiki na unazi wa kijinga?


Unaongelea vijiji gani hapa, vya pemba, tarime, kigoma au vya wapi?

Unaweza kunionyesha mahali kwenye katiba au ilani ya ccm panaposema kuwa sera ya ccm ni ufisadi?

Vitendo vinaongea zaidi kuliko maneno.

Chama hakiwezi kutoka mbinguni hata siku moja.Chama lazima kitoke tanzania na kitengenezwe na watanzania.Kitapatikana,mimi bado nina imani hiyo.Lakini kwa sasa bado hakipo.

na hao watanzania wewe ni miongoni mwao, je umeanzisha chama karibuni?


Umakini wa chama ni pamoja na kuuza nchi, kuiba pesa BoT, kutojali wananchi kwa standard zako?
 
Hivi mwenye mcho ataammbiwa tazama?? Kwanza chaguzi za ndani za ccm ni zengwe kuliko la mlingotini...
Rushwa, kuchafuana hata muda mwingine hutishia uhai wa watu... kisa? MADARAKA

Hawa ccm watatawala mpaka watakapoondolewa kwa kura zetu kwani kuongoza waliacha zamani sana....
 


[]NI LINI TENA WAKEREKETWA WA VYAMA VYA SIASA WAMEVAMIA HAPA JF. HAPA JF HAKUNA UKEREKETWA WA VYAMA VYA SIASA BALI:

ukereketwa wa utaifa wetu, taifa langu la tanzania ambalo nina madeni mengi juu yako, kama vile kwa kushindwa kukupigania wewe hadi mbwa mwitu wakakuzonga, wakakunyanganya tonge lako mdomoni, na tazama ehe tanzania, wanao wanafia kwenye mapokezi ya hospatali kwa kukosa wembe na sindano za kujifungulia, wakati mbwa mwitu wanaficha mamilioni nje ya mipaka yako.

sisi hapa si wakereketwa wa vyama vya siasa, kwa kuwa ni vikundi vilivyoanzishwa na binadamu kwa matakwa ya binadamu, navyo hufa na kusahaulika, lakini sisi ni wakereketwa wa taifa letu tulilopewa na Mungu lipo milele

sisi si wakereketwa wa vikundi vinavyoitwa vyama vinavyojitambulisha kwa rangi za bluu, kijani, njano, kwa kuwa chini ya rangi hizi ni vivuli vya majambazi yenye maalengo na kiu ya ujambazi kama vile kunguru anavyotamani vijito vya maji

ENYI WASOMI WA NCHI HII, TAMBUENI NA AMKENI KWENYE BLANKETI ZITO LIITWALO VYAMA, MMEFUNIKWA MSILIJUE TAIFA LENU

Mara ngapi mafisadi wamejificha kwenye mapazia yaitwayo vyama. kama siyo vyama kuwalinda mafisadi je wangekuwa wapi leo?

wiliam shakespear- ni nani mjinga kiasi hicho mpaka alisahau taifa lake?
 

Hiyo siku inakuja na si mbali sana.. jitihada zinazofanyika hapa na msaada wote tunaopata kwa wenye magazeti nyumbani na ambao wanaandika uozo wa ccm day after day wanasaidia kuelemisha watanzania taratibu.

Kwa kadri mafisadi wanavyoishiwa hapa JF na kubaki kuweka viroja, wataishiwa hata huko nyumbani one of these days. Malalamiko na vilio vya watoto wachanga vinamfikia MUNGU na kuna siku ataamua kukomesha ufisadi wa ccm.

Hiyo siku inakuja na haiko mbali!....
 

Ahsante, Mwafrika wa Kike.

Na na mimi mara nyingi najisikia kutapika neno 'Sisiemu' likitajwa. Natamani nijichimbia ardhini mpaka nisikie CCM imeondoka juu ya uso wa dunia ndo niibuke tena duniani kama Michael Jackson kwenye filamu ya Threaller!

Lakini naomba kupata wazo lako jingine kuhusu sera inayosema "chochote ila CCM."

Ni sahihi nikitafsiri kwamba sera yako inasema "upinzani unafaa kwa sababu CCM haifai"?
 
\

kwi kwi kwi mkuu wangu!

You can make your own call baada ya kuitapika ccm
 
Una hakika kuwa hupendi unafiki na unazi wa kijinga?
 

Mungu achagui anawaona mafisadi wote, wa ccm, chadema nk.
 
Huwa natenda ninalohubiri.Afterall kigumu kiko wapi?Kwani wewe mwkike huwezi kuishi bila unafiki na unazi wa kijinga?

Hilo ni swali ambalo una jibu lake kwa vile wewe ndio umeleta hapa maneno hayo - unazi wa kijinga

Hayo ya pemba yaache kabisa.siasa za zanzibar zina historia yake hivyo ni tofauti kabisa na za bara.Na wenyewe idadi yao ni ndogo sana kuwafanya ccm bara wakose ushindi.Kwahiyo ushindi wa wapemba usikufariji sana.

Ukishaanza kutenganisha sehemu fulani na kuzihesabu kuwa sio sehemu ya Tanzania au kuwa sio vijijini basi unarudi pale kwenye suala la upeo wako wa kuelewa!


Rudi tena usome statements zako maana inaonekana short memory yako ina matatizo kidogo.

Sina uwezo wa kuanzisha chama cha siasa.

Kama huna uwezo wa kuanzisha chama then unategemea nani akuanzishie huyo mwenye uwezo wa kuanzisha vyama?
 
Mungu achagui anawaona mafisadi wote, wa ccm, chadema nk.

Especially mafisadi waliiofanya yafuatayo

kusaini mkataba mbovu wa Buzwagi, Richmonduli, wizi BoT, Kiwira, IPTL, Bulyanhulu, na kununua rada feki, ndege ya bei ya kutupwa, na kupelekea ukosefu wa huduma muhimu nchini kwa watanzania - wana ccm
 
Hilo ni swali ambalo una jibu lake kwa vile wewe ndio umeleta hapa maneno hayo - unazi wa kijinga


Kuwa na uwezo wa kuanzisha chama isiwe sababu ya kutuletea vyama chungu nzima visivyo na kichwa wala miguu vilivyojaa wababaishaji,waganga njaa,wanafiki,mamluki nk nk
 


Kuwa na uwezo wa kuanzisha chama isiwe sababu ya kutuletea vyama chungu nzima visivyo na kichwa wala miguu vilivyojaa wababaishaji,waganga njaa,wanafiki,mamluki nk nk

Ambao ni tofauti na waliofanya yafuatayo:

kusaini mkataba mbovu wa Buzwagi, Richmonduli, wizi BoT, Kiwira, IPTL, Bulyanhulu, na kununua rada feki, ndege ya bei ya kutupwa, na kupelekea ukosefu wa huduma muhimu nchini kwa watanzania - wana ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…