unajua sina mazoea na wewe, lakini kwa hili sikuweza kuacha liondoke, unaweza kuniambia ni nani niliyemtukana humu ndani ya forum ? au kama kuna yeyote niliyemtukana basi ajitokeze ! LINI ulishawahi nisikia kuna double standards, na kama nilisema je ulielewa nilichokuwa nakiongelea ?
anyway tuendelee kujadili vyama feki ambavyo vimejaa rundo tanzania na tuvikemee !
Ndiyo kuna member humu ndani ulimwita Ignorant kwenye ile thread ya jana ya 'WANAJF"
Pia kuna mahali ulimtukana mwafrika wa kike.
Ndiyo maana nikafikiria mtu mwenye akili timamu hawezi kutukana hovyo hapa unless unakula Jani.
Kuhusu kujadili vyama feki Tanzania,
naanza Na CCM.
CCM ni CHAMA feki kuliko Vyote Tanzania kutokana na kuwa chimbuko la umaskini wetu.Hawa ndio wako responsible kwa
-Huduma duni za afya na elimu
-Ukosefu wa ajira klwa vijana kutokana na sera mbovu za ubinafsishaji
-Chanzo cha maovu yote kamavile Uchangudoa,ujambazi na uharamia kutokana na wananchi kuwa maskini kotokana na sera mbovu za CCM
-Vijana wengi kukosa elimu bora na pia CCM ndio chanzo cha ongezeko la watoto wa mitaani ambao wengi utakuta ni yatima kutokana na wazazi wao kujihusisha na biashara haramu za kujiuza,au wazazi wao kuwatoroka au kuikana familia kutokana na hali duni ya maisha ambyo tumesababishiwa na hicho chama feki kilichokaa madarakani tangu uhuru kupitia Tanu na kisha CCM yenyewe.
- Leo hii Kenya wametugeuza soko lao kutokana na sisi kuwa nyuma kiuchumi,CCM kwa kweli wako responsible kupotea kwa heshima ya taifa letu.
- Mianya mingi ya ukandamizaji katika mfumo wetu wa mahakama umesababishwa na Hiki chama feki CCM kwani ni chama ambacho hata kunyoosha system yetu ya mahakama kilishindwa kwani hiki ni chama ambacho kina hitoria ya Kunakili vitu na kuiga tu.Sanaa yao kubwa hata ktk sera zao wenyewe ni katika COPY and PASTE technology
-Kwa kweli hiki Chama kimeota mizizi ya ufisadi kwani tangu wanachama wake waliopewa dhamana ya kuongoza wizara mbalimbali walipokabiliwa na tuhuma za Rushwa,basi kutokana na ufeki wa hicho chama hakijawahi hata siku moja kujitokeza na kuwahoji hao Mafisadi ili kutufanya sisi wananchi tuamini kwamba hakijahusika na ufisadi.
Hayo hapo juu ni machache tu.Sijui kada na wenzako mko nchi gani kama haya yote hapo hamuyaoni.Najua mtaleta mashambulizi ya kijinga lakini jibuni hoja ili msije kuthibitisha ufeki wenu zaidi hapa.
Heshima mbele!