Hali ni mbaya sana, makosa aliyoyafanya Nyerere sasa yameanza kuleta matokeo.
Wakati tunaingia kwenye mfumo wa vyama vingi Nyerere alikuwa na ushawishi mkubwa sana, licha ya kwamba 80% hawakutaka mfumo wa vyama vingi, Nyerere alilazimisha. Tukaingia kwenye mfumo tukiwa na katiba ya mfumo wa chama kimoja, hili likawa kosa namba moja.
Kosa namba mbili ilikuwa ni kukiacha chama kongwe kishindane na vyama vichanga. Ilitakiwa CCM ifutwe, wote waanze mchakato wakiwa vyama vichanga.
Sasa CCM haitaki kusikia upinzani, kila kukicha wapinzani wanatekwa, wanauliwa na kuteswa.
Wananchi hatutakiwi kukosoa wala kujiunga na upinzani, maana kuwa upinzani ni kujisogeza kaburini.
Tumshauri mama afute vyama vyote vya upinzani, tubaki na CCM tu, hapo ndio salama yetu itarejea.