Vyama vya Upinzani vilimtoa Jasho Hayati Magufuli. Je, upinzani ndani ya CCM, Serikali na Vyama vya Upinzani Rais Samia atauweza?

Uongozi siyo mabavu, matusi, kufoka au kuongozana na IGP au CDF kama alivyokuwa anafanya Magufuli. Instead uongozi ni karama ambayo mtu anazaliwa nayo, hekima na busara ya kuwashirikisha wengine katika maamuzi. Magufuli hakujaaliwa karama hizo.

Rais Samia amejaliwa vyote hivyo PLUS kuwa ni mpenda haki, mkweli na mcha Mungu kwa matendo.

Tayari Samia ameituliza nchi, upende usipende. Ule UHAYAWANI wa kutekana na kuuana haupo tena. Vyama vinafanya mikutano yao na uhuru wa maoni unaheshimiwa
 
Busara hizo hizo ziendepee kuhakikisha tunapata tume huru ya uchaguzi na Katiba Bora

Hongera sana kwake kama hivyo ulivyotaja anavyo.
 
Je ndani ya chama atakubali kupingwa?
Ndo hapo akilazimisha unafanyika Utaratibu Ule uliozoeleka,

Asubuhi CCM jioni mtu yule yule unamkuta akitoa Siri zote upinzani!!

Upendo haununuliwi Kwa pesa.

Pia kumbuka, CCCM niijuayo haijawahi kuleta mgombea asokubalika machoni pa umma.
 
Ndo hapo akilazimisha unafanyika Utaratibu Ule uliozoeleka,

Asubuhi CCM jioni mtu yule yule unamkuta akitoa Siri zote upinzani!!

Upendo haununuliwi Kwa pesa.
Hehehee
 
Uko sahihi kwa sababu kama sikosei bado wasukuma wanaamini kuwa Hayati Magu aliuawa! Sasa Lissu kwa kauri zake bila kujua anatonesha vidonda vyao!
 
Uko sahihi kwa sababu kama sikosei bado wasukuma wanaamini kuwa Hayati Magu aliuawa! Sasa Lissu kwa kauri zake bila kujua anatonesha vidonda vyao!
Mbona kanda ya ziwa wameshamwelewa Lissu? Au hufatilii siku hizi?
 
Pamoja na uwepo wa vyama vingi katika ushindani wa kuunda serikali na kuongoza nchi, kitu muhimu ni siasa za ukweli wenye kutumia akili chanya kwa maendeleo na mustakabali mwema wa wananchi na vizazi vijavyo.
Haina maana kabisa kama tutafikiria kuhusu vyama tu huku taifa likiangamia (ubinafsi).
Hata hivyo, Rais Samia alikuja na R zake ili kupunguza huo ubinafsi kwa kuangalia vyama. Changamoto itakuwa utekelezaji kwa kuwa wazo ni nzuri ila wabinafsi na wachoyo ni wengi watakaomzunguka.
 
Sahihi......ndio maana vyama vinahesabika kuwa ni viwili tu. Huo utitiri mwingine ni kupoteza maboya. Ni ccm na chadema tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…