Vyama vya Upinzani vilimtoa Jasho Hayati Magufuli. Je, upinzani ndani ya CCM, Serikali na Vyama vya Upinzani Rais Samia atauweza?

Vyama vya Upinzani vilimtoa Jasho Hayati Magufuli. Je, upinzani ndani ya CCM, Serikali na Vyama vya Upinzani Rais Samia atauweza?

Ni wazo tu. Tujaribu kuwaza kwa pamoja kwenye siasa za Tanzania.

Rais Dkt. Samia ni Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ambapo kwa mujibu wa Katiba Yao wanasema Rais akianA awamu ya kwanza sharti apewe nafasi kuendelea na kipindi cha Pili. Lakini wenye macho na masikio tumeona kuna vugu vugu la upinzani ndani ya Chama chake wako tayari kutoa upinzani wakati wa Uchaguzi unaotarajiwa 2025.

Licha ya hivyo tumeshuhudia wimbi kubwa la wanachama damu damu wa ccm na kundi kubwa la wananchi wasio na vyama wakipinga sera zake wazi wazi.

Moja ya jambo ambalo limezua seke seke ni hili la bandari pamoja na mambo mengine

Hapo hapo tukikumbuka jinsi Hayati Dr John Pombe Magufuli alivyotoka jasho kudhibiti Upinzani wa vyama vya upinzani je huu upinzani uliounganika Dr Samia Suluhu Hassani atauweza?

Ikumbukwe siasa za wakati wa leo zimebadilika sana tofauti na miaka 5 au 10 iliyopita.
Uongozi siyo mabavu, matusi, kufoka au kuongozana na IGP au CDF kama alivyokuwa anafanya Magufuli. Instead uongozi ni karama ambayo mtu anazaliwa nayo, hekima na busara ya kuwashirikisha wengine katika maamuzi. Magufuli hakujaaliwa karama hizo.

Rais Samia amejaliwa vyote hivyo PLUS kuwa ni mpenda haki, mkweli na mcha Mungu kwa matendo.

Tayari Samia ameituliza nchi, upende usipende. Ule UHAYAWANI wa kutekana na kuuana haupo tena. Vyama vinafanya mikutano yao na uhuru wa maoni unaheshimiwa
 
Uongozi siyo mabavu, matusi, kufoka au kuongozana na IGP au CDF kama alivyokuwa anafanya Magufuli. Instead uongozi ni karama ambayo mtu anazaliwa nayo, hekima na busara ya kuwashirikisha wengine katika maamuzi.

Rais Samia amejaliwa vyote hivyo PLUS kuwa ni mpenda haki, mkweli na mcha Mungu kwa matendo.

Tayari Samia ameituliza nchi, upende usipende. Ule UHAYAWANI wa kutekana na kuuana haupo tena. Vyama vinafanya mikutano yao na uhuru wa maoni unaheshimiwa
Busara hizo hizo ziendepee kuhakikisha tunapata tume huru ya uchaguzi na Katiba Bora

Hongera sana kwake kama hivyo ulivyotaja anavyo.
 
Je ndani ya chama atakubali kupingwa?
Ndo hapo akilazimisha unafanyika Utaratibu Ule uliozoeleka,

Asubuhi CCM jioni mtu yule yule unamkuta akitoa Siri zote upinzani!!

Upendo haununuliwi Kwa pesa.

Pia kumbuka, CCCM niijuayo haijawahi kuleta mgombea asokubalika machoni pa umma.
 
Ndo hapo akilazimisha unafanyika Utaratibu Ule uliozoeleka,

Asubuhi CCM jioni mtu yule yule unamkuta akitoa Siri zote upinzani!!

Upendo haununuliwi Kwa pesa.
Hehehee
 
Binafsi mimi sio mtu wa siasa sana lakini kuna kitu niwaambie tu Chadema waitumie vizuri hii fursa iliyopo wakati huu kanda ya ziwa,, hakuna mtu anayeitaka CCM nawaambia ukweli,, muhimu viongozi wa Chadema wajitahidi kumdhibiti Lissu asiendelee kumsema Magufuli hapa tu basi,, kuendelea kwake kumsema kwa mabaya Magufuli licha tu ya kuwa sio utamaduni wa wasukuma bali pia kunafifisha hata ule udogo wa imani waliyonayo juu yake,, amuache mzee wetu apumzike kwa amani,, kura zote za kanda ya ziwa ziko wazi kwa yeyote atakaye kuwa serious na maisha yao,,
Uko sahihi kwa sababu kama sikosei bado wasukuma wanaamini kuwa Hayati Magu aliuawa! Sasa Lissu kwa kauri zake bila kujua anatonesha vidonda vyao!
 
Uko sahihi kwa sababu kama sikosei bado wasukuma wanaamini kuwa Hayati Magu aliuawa! Sasa Lissu kwa kauri zake bila kujua anatonesha vidonda vyao!
Mbona kanda ya ziwa wameshamwelewa Lissu? Au hufatilii siku hizi?
 
Pamoja na uwepo wa vyama vingi katika ushindani wa kuunda serikali na kuongoza nchi, kitu muhimu ni siasa za ukweli wenye kutumia akili chanya kwa maendeleo na mustakabali mwema wa wananchi na vizazi vijavyo.
Haina maana kabisa kama tutafikiria kuhusu vyama tu huku taifa likiangamia (ubinafsi).
Hata hivyo, Rais Samia alikuja na R zake ili kupunguza huo ubinafsi kwa kuangalia vyama. Changamoto itakuwa utekelezaji kwa kuwa wazo ni nzuri ila wabinafsi na wachoyo ni wengi watakaomzunguka.
 
Sahihi......ndio maana vyama vinahesabika kuwa ni viwili tu. Huo utitiri mwingine ni kupoteza maboya. Ni ccm na chadema tu.
 
Back
Top Bottom