Vyama vya Wafanyakazi Tanzania ni Kansa kwa Wafanyakazi

Vyama vya Wafanyakazi Tanzania ni Kansa kwa Wafanyakazi

Black Legend

Senior Member
Joined
Jul 28, 2015
Posts
174
Reaction score
301
Kwa muda mrefu nimefanya personal study kuhusu ubora na dhima ya vyama vya wafanyakazi Tanzania vikiongozwa na chama mama TUKTA na kuja na hitimisho kuwa , VYAMA VYA WAFANYAKAZI TANZANIA NI KANSA KWA WAFANYAKAZI. Kwa kuangalia haya machache ni dhahiri kuwa msaada wake kwa wafanyakazi ni sawa unafki, unyonyaji na ulaghai mkubwa.

1. Wafanyakazi Wana madai ya miaka Mingi lakini vyama hivyo havioneshi msaada katika kushughurikia hilo.

2. Kukusanya fedha viwango vikubwa toka kwa wafanyakazi pasipokuwa na ajenda zenye matokeo chanya kwa wafanyakazi(Mfano CWT, TUGHE....nk).

3. Kujitokeza kudai HAKI za wafanyakazi kwa siku moja tu (MEI MOSI)...hapa ndipo utaona unafiki wa vyama hivi.
4. Viongozi wake kutumika kisiasa.

5. nk.
 
Yaani vyama hivi vipo kama vile vya hashimu Rungwe ,hamadi rashidi,lipumba vyenyewe kazi yake ni kusema ndio Kwa kila jambo
 
Back
Top Bottom