Soma sheria iitwayo "Master Servant Act" ya 1823. Ndiyo inayohusika bongoland.Kwanza nitangaze wazi kwamba Mimi ni Kiongizi Mwandamizi wa Chama cha wafanyakazi sekta ya Nishati na Madini (Sekta ya Uziduaji) Tanzania, kinaitwa kwa ufupi NUMET.
Pamoja na kwamba hatuhusiki sana na wafanyakazi wa sekta ya umma ambayo inalalamika sana kwasababu za kutoongezwa mishahara, na masilahi mengine, na sisi pia kwenye sekta binafsi wanachama wetu hawako na furaha kama tulivyotarajia au kama walivyotarajia.
Kuna mambo mengi tunafanya, Lakini kwasababu mbalimbali kuna mambo mengi hatujafanya. Lakini angalau kuna juhudi zinafanyika na baadhi ya wanachama wetu wanashiriki moja kwa moja.
Lakini, ukitafuta kiwango cha wafanyakazi nchini kuridhishwa na huduma zitolewazona vyama vya wafanyakazi nchini kwa ujumla wake, ni kidogo sana.
Jukwaa hili lina watu wenye uelewa wa mambo mengi sana. Mnafikiri vyama hivi vinakwama wapi? Maana kuendelea kulalamika tu bila kutoa suluhu inaweza isisaidie sana kujikwamua kwenye mkwamo huu.
Karibuni tujadili.
Nicomedes M Kajungu
Katibu Mkuu
NUMET
MWANZA HQ
T
Habari wanajukwaa! Nimekuwa nikitafakari kwa kina juu ya kazi za vyama vya wafanyakazi na mchango Wa vyama hivyo kwa wanachama wake yaani watumishi Wa Umma, kwa upande wangu sijaona kama vina msaada kwasababu watumishi hawapandi vyeo wala kupata ongezeko la kila mwaka yaani annual increment, cha ajabu watumishi bado wanaendelea kuwa wanachama. Vyama hivi kazi yake kubwa ni kuwanyonya wanachama wake badala ya kuwasaidia kupata stahiki zao, kwa jicho la tatu nahisi vyama hivi ni vibaraka vya serikali kuu na huenda wanakula pamoja. Huenda kuna wanachama wanaofaidika, naomba watupatie ushuhuda ili tusiendelee kuwa na fikra potofu. Naomba kuwasilisha.
Hivi vyama vya wafanyakazi kujiunga ni lazima na imefanywa kuwa lazima kwavile ni njia ya ulaji kati ya viongozi wa vyama na watawala wa nchi.
Yaani ujiunge usijiunge hela yako inakatwa direct kutoka hazina..
Sent using Jamii Forums mobile app
Kujiunga sio lazima ni hiyari. Na una haki ya kujitoa uanachama. Sio lazima ndugu kuwa mwanachama....Hivi vyama vya wafanyakazi kujiunga ni lazima na imefanywa kuwa lazima kwavile ni njia ya ulaji kati ya viongozi wa vyama na watawala wa nchi.
Yaani ujiunge usijiunge hela yako inakatwa direct kutoka hazina..
Sent using Jamii Forums mobile app
Labda vyama vingine ila cwt ni lazima ukishaajiriwa serikalini utake usitakeKujiunga sio lazima ni hiyari. Na una haki ya kujitoa uanachama. Sio lazima ndugu kuwa mwanachama....
Sent using Jamii Forums mobile app