Lissu ameshindwa kabisa kuunganisha makundi kwenye chama? Ni udhaifu mkubwa sana wa kiuongozi huu.
Sifa moja kubwa ya kiongozi bora ni pamoja na kuleta watu wote pamoja haswa katika kipindi hiki muhimu cha uchaguzi mkuu. Kama kiongozi alitakiwa kuhakikisha chama kwa vyovyote vile hapatokei mpasuko.
Ila pia hao G55 wana ubinafsi mkubwa sana. Sioni kama wanatetea muelekeo sahihi wa kulikomboa taifa katika kupata sera sahihi za uchaguzi huru na katiba mpya ya nchi
Zaidi wao wanachong'angania ni vyeo kama wasipogombea ubunge itakuwaje.
Viongozi MATUMBO yao kwanza! Wtanzania watawakataa!!