Vyeo vya Brigadier na Brigadier General vina utata kidogo na watu wengi hudhani kuwa ni cheo kimoja kwa vile nchi nyingi duniani hazivitumii vyote viwili pamoja; kama nilivyoonyesha kwenye list hiyo, Brigadier General yuko juu ya Brigadier. Kwenye nchi nyingi za Commonwealth, kasoro chache kama Canada, Tanzania na Uganda, hakuna cheo cha Brigadier General bali kuna Brigadier.
Marekani kama ilivyo kwa Canada, Tanzania, Uganda na nchi nyingi za kiarabu, hakuna cheo cha Brigadier bali kuna Brigadier General. Nchi kadhaa kama vile China hawana vyeo hivyo kabisa; kwa mfano China kutoka Colonel cheo kinachofuatia ni Major General (nyota moja) , Lt Gen (nyota mbili), General (nyota tatu) halafu wana cheo kingine juu ya General ikinatwa Full General ambaye ndiye ana nyota nne.
Hata hivyo kwenye majeshi ya nchi kadhaa kama vile Iran wanavyo vyote viwili. Iran wana Second Brigadier General (sawa na Brigadier) halafu ndipo anakuja Brigadier General. Nchi nyingi za Eastern Europe zilikuwa navyo vyote viwili kabla ya kujiunga na NATO; baada ya kujiunga na NATO waliondoa cheo cha Brigadier na kubakiza cha Brigadier General kuendana na vyeo vya Marekani.
Pamoja na kuwa Portugal imo ndani ya NATO, bado inavitumia vyeo vote viwili ambapo Brigadier General anaitwa Brigadeiro-general wakati Brigadier anaitwa Coronel-tirocinado ingawa mwanzoni alikuwa anaitwa Brigadeiro.
Kwa nchi za carribean na Amerika ya kusini nadhani ni Cuba tu ndiyo inavyo vyote viwili ingawa kwa majina tofauti pia; Brigadier General anaitwa General de brigada wakati Brigadier anaitwa Primer coronel. Kwa Africa nadhani ni nchi tatu tu zenye kutumia vyeo vyote viwili ambazo ni Mali, Corte d'Ivor, na Burkina Faso. Kwenye nchi hizo Bigadier General anaitwa Général de brigade wakati Brigadier anaitwa Colonel-major
La kuelewa ni kuwa Brigadier General ni tofauti na Brigadier ingawaje ni nchi chache zenye vyeo hivyo viwili kwa pamoja, na nchi kadhaa hazivitumii kabsa.