Vyeo vya Maafisa Jeshi vilivyopo na ambavyo havitumiki katika Jeshi la taifa kwa sasa

Topic inahusu maafisa wa jeshi kuanzia cadet officer. Haikusema vyeo vyote vya JWTZ

Vyeo vya maafisa wa JWTZ ni vile ambavyo havikuandikwa kwa rangi nyekundu. Soma post kwa makini uielewe kabla ya kuijibu bila kuelewa unachojibu.
Extended reply; litawasaidia wengine wanaohitaji kujifunza.
Kuna madhara yoyote kwa jibu hilo?
Samahani kwa usumbufu afande.
 
Elimu,
Elimu,
Elimu.
Mtililiko ❌❌
Mtiririko ✅✅

RIP Edward N. L
Una matatizo kama unadhani lafudhi au matamshi ya maneno kwenye lugha ndiyo elimu yenyewe. Tuliwahi kufundishwa kuwa elimu nusu ni sumu kwa sababu watu wenye elimu nusu hudhani wanajua sana kila kitu kuliko watu wengine wote.

Elimu yako ni ndogo sana kama hiyo ndiyo point uliyoona kwenye post yote
 
RIP Edward N. L.
 
Asante mkuu.

Kumbe mtu kuwa na Nyota sio mchezo.
Hawa Kaka zetu tunaona wana nyota na miili yao haiko sharp sana inakuwaje
 
Vyeo vya Brigadier na Brigadier General vina utata kidogo na watu wengi hudhani kuwa ni cheo kimoja kwa vile nchi nyingi duniani hazivitumii vyote viwili pamoja; kama nilivyoonyesha kwenye list hiyo, Brigadier General yuko juu ya Brigadier. Kwenye nchi nyingi za Commonwealth, kasoro chache kama Canada, Tanzania na Uganda, hakuna cheo cha Brigadier General bali kuna Brigadier.

Marekani kama ilivyo kwa Canada, Tanzania, Uganda na nchi nyingi za kiarabu, hakuna cheo cha Brigadier bali kuna Brigadier General. Nchi kadhaa kama vile China hawana vyeo hivyo kabisa; kwa mfano China kutoka Colonel cheo kinachofuatia ni Major General (nyota moja) , Lt Gen (nyota mbili), General (nyota tatu) halafu wana cheo kingine juu ya General ikinatwa Full General ambaye ndiye ana nyota nne.

Hata hivyo kwenye majeshi ya nchi kadhaa kama vile Iran wanavyo vyote viwili. Iran wana Second Brigadier General (sawa na Brigadier) halafu ndipo anakuja Brigadier General. Nchi nyingi za Eastern Europe zilikuwa navyo vyote viwili kabla ya kujiunga na NATO; baada ya kujiunga na NATO waliondoa cheo cha Brigadier na kubakiza cha Brigadier General kuendana na vyeo vya Marekani.

Pamoja na kuwa Portugal imo ndani ya NATO, bado inavitumia vyeo vote viwili ambapo Brigadier General anaitwa Brigadeiro-general wakati Brigadier anaitwa Coronel-tirocinado ingawa mwanzoni alikuwa anaitwa Brigadeiro.

Kwa nchi za carribean na Amerika ya kusini nadhani ni Cuba tu ndiyo inavyo vyote viwili ingawa kwa majina tofauti pia; Brigadier General anaitwa General de brigada wakati Brigadier anaitwa Primer coronel. Kwa Africa nadhani ni nchi tatu tu zenye kutumia vyeo vyote viwili ambazo ni Mali, Corte d'Ivor, na Burkina Faso. Kwenye nchi hizo Bigadier General anaitwa Général de brigade wakati Brigadier anaitwa Colonel-major

La kuelewa ni kuwa Brigadier General ni tofauti na Brigadier ingawaje ni nchi chache zenye vyeo hivyo viwili kwa pamoja, na nchi kadhaa hazivitumii kabsa.
 
Uko vizuri, ingawa hicho namba 3 kwasasa ni kama hakipo
 
Tanzania hakuna brigedia Mkuu kuna brigedia generali
 
Marco Gaguti alikuwa na cheo gani kipindi anahudumu uRC?
 
Major ni mkubwa kuliko Lieutenant,
Lakini Lieutenant General ni mkubwa kuliko Major General!
Kwanini Iko hivi?
 
Major ana ngao ya bibi na bwana mabegani, Luteni ana nyota mbili.

Luteni General, ana bibi na bwana, nyota tatu na mkasi.

Major General, ana bibi na bwana, nyota mbili na mkasi.
majibu mepesi haya hata aliyeuliza swali atakuwa anayajua, hebu jikite kwenye majibu ambayo hatuyajui.
 
Brigadier
Hawa mbona wapo Tanzania au walifutwa
Ningeshauri ikikupendeza kwenye brackets au kwa bullet points uweke hivyo vyeo vinatamkwaje kwa lugha zote mbili, vyeo wanavyovaa mf idadi ya nyota, crown kwenye magari yao ikiwezekana na majukumu yao
 
Hii ndiyo nami naifahamu, nimeshangaa yeye anasema Brigadier haipo Tz akaiweka in red!!
 
Kumbe kati ya Major General na General, General ndio mkubwa?
 
Hawa mbona wapo Tanzania au walifutwa
Ningeshauri ikikupendeza kwenye brackets au kwa bullet points uweke hivyo vyeo vinatamkwaje kwa lugha zote mbili, vyeo wanavyovaa mf idadi ya nyota, crown kwenye magari yao ikiwezekana na majukumu yao
Hapa; Brigadier no tofauti na Birgadier General; in fact Brigadier General yuko juu ya Brigadier. Kuna post nyingine nimeeleza tofauti za vyeo hivyo kwani wengi hudhani ni cheo kile kile. Tanzania tuliporithi mfumo wa Kiingereza tulikuwa na brigadier, lakini baadaye tulifanya transition kwenda mfumo wa kimarekani kama ambavyo Kanada na Uganda pia zilifanya, tukaondoa cheo cha Brigadier na kuweka Brigadier General. Wale waliokuwa Mabrigadier wakati huo wakapanda kuwa Brigadier General. Kenya na India bado wanafuata vyeo vya kiingereza hivyo wao wana brigadier.

Soma post hii

 
Hii ndiyo nami naifahamu, nimeshangaa yeye anasema Brigadier haipo Tz akaiweka in red!!
Nimeandika vyeo vya maasifa wa jeshi na nilitaka kusisitiza vyeo ambavyo havitumiki Tanzania kwani vyeo vingine vilishwahi kutajwa humu siku nyingi sana; soma title vizuri haisemi vyeo vya kijeshi mbali inasema vyeo vya maafisa wa jeshi. Yeye ameunganisha na vyeo vya NCOs ambavyo pia vilishawahi kuandikwa humu siku nyingi sana. Na labda hujui kuwa NCOs siyo maafisa wa jeshi wala hawezi kwenda kula "Officers' Mess". Jeshi la urusi halina hao NCOs kabisa. Halafu vyeo vha NCOs havita utaratibu maalumu. Kuna nchi nchingine zina Searganet wa level nene hadi tano; Warant Officers Class nne, Nchi nyingi hazina lance corpolar, lakini zina Private, Private first class, Specialist, Bombadier na ngazi mbalimbali za Private ndiyo maana hakukuwa na haja kuviweka hapa kama nia ilikuwa ni kuonyesha vyeo visivyotumika Tanzania.

Tanzania hakuna brigadire bali kuna Brigadier General. Zamani tulikuwa na Bridagire lakini baadaya cheo hicho kikafutwa kikwekwa cha Brigadier General. Halafu Brigadier siyo Brigadier general.

Soma hapa

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…