Vyeti feki na nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma; kwavyo nitakukumbuka

Vyeti feki na nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma; kwavyo nitakukumbuka

DustBin

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2021
Posts
609
Reaction score
604
Nawasalimu kwa jina la JMT

Moja kwa moja niende kwenye mada.

Leo nimeamkua na kukumbuka namna watumishi wa vyeti feki walivyokua wameziba nafasi za ajira kwa wenye sifa. Dhulma hii ikasawazishwa kwa kuondolewa waliobainika kughushi taarifa za ajira hasa kwenye vyeti vya taaluma.
Heko..! Kwa waliosimamia hili ingawa kuna ambao waliumia na kuendelea kuumia mpaka leo.

Jambo la pili ni namna ambavyo watoa huduma kwenye taasisi za umma mbalimbali walivyokua na nidhamu kazini, na zile dharau zilipungua kwa kiasi kikubwa mno, kiasi mteja kweli alikua mfalme.
Nimeona maeneo fulani kuna viashiria vya baadhi ya watumishi kujiachia na kufanya Business As Usual (BAU). Wito kwa wahusika wawe macho ktk hili, hawa wachache wasije tuharibia mfumo wetu ulioundwa kwa gharama kubwa.

Kwa haya nitamkumbuka daima.


Ndimi
Mpenda haki na uadilifu
DustBin
 
Magufuli alikuwa ni mnafiki na mjinga anaetetea maslahi yake binafsi ndiyo maana kwenye ishu ya vyeti fake hakumgusa Bashite.
 
Magufuli alikuwa ni mnafiki na mjinga anaetetea maslahi yake binafsi ndiyo maana kwenye ishu ya vyeti fake hakumgusa Bashite.
Pamoja na mapungufu hayo yote, lakini lile zoezi la kuwaondoa madhalimu anastahiki heko
 
Kwenye kuziba ajira hapo umetupiga na kitu kizito, Pamoja na kuondolewa vyeti feki hakukuwa na mbadala wa kuongeza watumishi bali lengo lilikuwa kupunguza idadi tu ili wahangaike kufanya kazi nyingi wafanyakazi waliopo
 
Pamoja na mapungufu hayo yote, lakini lile zoezi la kuwaondoa madhalimu anastahiki heko
Hakuondoa madhalimu.Madhalimu kama vile akina Bashite wenye vyeti fake aliwaacha serikalini.

Magufuli ni DustBin ambalo halipaswi kukumbukwa katika Historia ya nchi hii.
 
Back
Top Bottom