Vyeti feki na watumishi hewa ilikuwa changa la macho

Vyeti feki na watumishi hewa ilikuwa changa la macho

Joined
Jul 11, 2020
Posts
66
Reaction score
145
Sakata la vyeti feki na wafanyakazi hewa ni moja kati ya suala ambalo lilishika sana vyombo vya habari mwanzoni mwa mwaka 2017. Katika makala haya naangalia kama yalileta matokeo chanya kwa kudhibiti mishahara kwa wasio stahili na mishahara hewa

Mwaka 2019 waziri Mkuchika alisema Serikali ya Awamu ya Tano ilifanikiwa kuwaondoa kazini watumishi hewa na wenye vyeti feki zaidi ya 40,000, aliyasema hayo Desemba 11, akiwa Dodoma katika kongamano la maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu

Serikali inatumia zaidi ya Tsh Bilioni 500 kwa mwezi kulipa mishahara kwa watumishi elfu 40 ambao walifukuzwa kazi tulitegemea kushuka kwa fedha inayotumika kulipa mishahara, kwa takwimu zilizopo fedha za mishahara zilishuka kidogo na kuanza kuongezeka kwa kasi

1626358547400.png

Graph ya Malipo ya mishahara kwa mwezi

1626358558900.png

Graph ya mishahara kuanzia mwaka 2015

Takwimu za mwezi zinaonesha fedha inayolipwa kwa mshahara kwa mwezi ilipanda na kushuka ghafla mwaka 2018 na kuongezeka taratibu kiasi ambacho mwaka 2019 serikali ikarudi kwenye kiwango kikubwa cha kulipa mishahara kuliko kilichokuwa awali

Mbali na ongezeko hilo la malipo ya mshahara, si kweli kwamba serikali imeajiri watu kwa kiwango cha watumishi walioondolewa, na kama iliajiri basi kuna shida ya kupanda kwa malipo ya mshahara ikiwa hakukuwa na ongezeko la mishahara kwa watumishi wa umma

Je, vyeti feki na wafanyakazi hewa ilikuwa ni bosheni?

Kwa graph hii inaonesha tofauti ya mishahaa kwa kila mwezi uliofuata ambapo mwaka 2018 ndipo malipo ya mshahara yalishuka kwa kiasi kikubwa kisha yakarudi kuwa chanya kwa maana malipo ya miezi iliyofuiata yalikuwa makubwa kuliko mwezi ulitangulia

POINT YA MSINGI
  • Mishahara haikupandisha kwa miaka mitano
  • Watumishi hewa na wenye vyeti walitimuliwa
  • Hakukuwa na ajira mpya kwa wengi
Lakini bado malipo ya mishahara kwa serikali yalipanda, Watumishi hewa bado ni shida au kuna watu bado wanakula visivyo halali


Data Source: BoT
 

Attachments

Kuna vingi sana ambavyo haviwez jibika...
 
Anaeweza kujibu hayo maswali ni hayati maguful mwenda zake...sisi wengine ukituuliza unatuonea bure
 
Vyeti feki ilikuwa ni kumridhisha bashite baada ya kunangwa na gwajima baba yake akaamua kumlipizia kizazi zama zile ndumba hazijaexpire bado.
 
Back
Top Bottom