Mwana Jf, kwanza pole sana kwa fikra hizi ambazo tulikaririshwa na waliotutangulia. ukweli ni kwamba watu tulio wengi huwa tunajua kuwa na vyeti vingi vilivyonakishiwa na maneno kama merit,excellent, first class ni basi. au tukiwa na prefix zinazotangulia majina au vyeo vyetu kama Dr. ms imetosha. Maisha hayako hivyo.kwenye jamii unayotakiwa kuishi kinachokutambulisha wewe ni uwajibikaji bora na uelewa mzuri wa mambo. kitu ambacho hakuna anayepewa phd au ms kwa kuwa navyo. hivi unatakiwa uwe navyo wewe mwenyewe kama mtu. elimu ya shule inakupa uwezo tu kupambanua mambo bali elimu ya uelew unaipata kwa bidii zako binafsi mathalan kwa kupenda kusikiliza wengine wanapoongea, kusoma vitabu, magazeti na hata kupenda kuandika.
mfano mzuri kuna mtu anaweza kusema kwanini niingie Jf lakini akawa amesahu kuwa hata kuweza kujiregister tu na mod akakujibu amefuta ujinga fulani akilini mwake, au pia akasahau kuwa kujadili hoja humu kunahitaji uwe na facts na uwe unayeweza kupangilia mawazo yako. Mara nyingine kupenda kukaa na watu wana jadili mambo tofauti tofauti yenye mantiki kunaongeza uelewa na unapochangia mada zao unajipa ujasiri nafsini mwako.
pia kuna kitu ambacho kimejengeka miongooni mwa wasomi wengi nacho ni kuwa na hofu na usomi wao, ukitaka kuamni kuwa usomi wako ni kitu kizuri basi utumie katika kujadili mada zilizoko ndani ya elimu yako, na siri moja nikupe siku zote tafuta reference ya vitu unavyovijua ambavyo utaweza kuvitetea. kamwe usilogwe kuongelea kitu ambacho huna reference yake nzuri, ukifanya hivyo itakupunguzia nafasi yako ya kuitetea point yako na mwisho ukajiona kama hujui mambo.
iwapo mada inayoongelewa siyo ndani ya uwanja wako wa kujidai basi hapo wewe penda kuuliza maswali zaid, na kusikiliza na hakikisha kuwa kila swali unaloliuliza linajenga kitu katika ufaham wako.kamwe usidharau hata kama anayeongea anaonekana kama vile siyo muelewa sana lakini ata kuongezea ufahamu kwenye fikra zako.
tabia ya kusoma nayo ni nzuri sana, soma as much as possible as you can. ukiona unaboreka sana tafuta mada kwenye jamvi zisome kwa makini kisha changia kwa kufuata lead(sijui kama unanielewa vizuri) ila kama hutanielewa sema nikueleweshe zaidi. sikiliza na angalia tv kwa ajili ya kujipa exposure. hapa utajifunza namna ya kuongea mbele za watu na jinsi unavyotakiwa kuongea. Watu wengi huwa hawajui kutofautisha namna ya kuongea na watu tofauti. Mathalani unavyoongea na marafiki, ni tofauti na classmate au na mtu anayetaka kujua jambo fulani na pia ni tofauti na unavyoongea na bosi wako au mteja au hata kiongozi wako. sasa yakupasa uue kundi unaloongea nalo kwa wakati huo ni lipi na unaongea nalo kitu gani. haya ukiyajua utajua uongee vipi kwa mahadhi gani.
kuhusu Lugha huo ni ugonjwa but one thing which i trust in shaping grammer is reading. read as much as possible as you can. read not only academic materials but also novels journals andmagazines anad news papers. while reading try to practice it do not hesitate and while doing it accept corrections. a single correction from a knowledgable person will prevent you from hundred mistakes. do not feel that you are humiliated when others are correcting you.
kama wewe ni mwaji wa kahawa au chai ya jioni basi nenda kapate katika mgahawa ambao utakutana na watu wanaojadili mada zitakazo kujenga kiakili. na uwapo hapo wewe uwe msikilizaji na muuliza maswali zaid kuliko kuwa masemaji.
Usiogope unapokosea hata kidogo kwani katika maisha mimi huwa ninaiambia nafsi yangu kwamba kila siku mimi huwa nina kosea sana au huwa nina tenda makosa mengi lakin pia kila siku huwa najifunza jambo jipya. na huwa kila ninachojifunza kinanikuza kiakili. changamoto ni lazima katika maisha usiziogope ila fungua akili yako na kuanza kutafuta maarifa ya uhalisia zaid kuliko yale ya kinadharia uliyoyapata ulipokuwepo shule.
usione kama ulikosea kusoma lahasha ila tu ulisoma kinadharia zaid kuliko kivitendo jambo ambalo hukuweza kuelewa mambo ya mtaani yakoje. Nafikiri ulipokuwa shule hukujua kuwa huku mtaani unaweza ukawa unakaa na watu ambao hata shule hawajaenda lakin wana heshima kuliko wewe na elimu yako.