Vyombo vya Dola havipaswi kuwa sehemu ya Maumivu ya Taifa

Vyombo vya Dola havipaswi kuwa sehemu ya Maumivu ya Taifa

Chikumba one

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
1,009
Reaction score
1,642
Kesi ya Mdude inaonyesha namna mtawala aliyetangulia alivyotumia vibaya vyombo ya Dola kupambana na Wapinzani WAKE. Ndio, ni Wapinzani WAKE, sio Wapinzani wa Nchi.

Hawa wote wanaoonekana hawana hatia leo bila shaka yoyote waliteswa kwa maelekezo yake.

Ni bahati mbaya sana mtu aliyewatesa Watanzania wenzake eti anaitwa Mzalendo.

Jeshi la polisi limejiweka katika wakati mgumu sana baada ya mtawala yule kuondoka.

Mahakama inatumia nafasi hii kujisafisha na mikono michafu waliyoshikwa miaka 6 ilopita.

Sijui jeshi la polisi litafanya nini kujisafisha.

Bila shaka linahitaji msaada wa kujisafisha.

Ni Mheshimiwa Rais Samia Suluhu pekee mwenye nafasi hiyo.

Ngoja tusubiri kuona atafanya nini zaidi.

Sijui wale makamanda wa polisi waliojitokeza kila mahali kwenye vyombo vya habari kutangaza tuhuma haramu dhidi ya Watanzania wenzao kwa sasa wanajisikiaje. Wale mawakili wa Serikali waliotumika kuwaangamiza Wapinzani wa Kiongozi yule wanajisikiaje kwa sasa?

Hakuna jambo baya kama kutumia taaluma yako kuwaangamiza wengine.

Wengi wameumizwa, maisha ya wasio na hatia yamepotezwa sababu ya ulevi wa madaraka. Binti mdogo Akwilina ni mojawapo ya mifano mibaya kabisa ya matukio hayo haramu.

Kiongozi aliyeasisi ubaya ule hastahiki kabisa kuitwa Mzalendo. Wazalendo hujitahidi kuliponya Taifa, sio kuliumiza Taifa.

Siku sio nyingi Mama Samia anaweza kuwa Mzalendo halisi kuliko yule tunaelazimishwa kuimba sifa zake.

Ukatili na kuogopwa kamwe haviwezi kuwa sehemu ya haiba ya Viongozi Wazalendo..

Vyama vyote vya siasa vinapaswa kuwa makini sana vinapoteua watu wa kusimamia nafasi za Uongozi wa Taifa letu. Hili ni muhimu sana.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Toka aendezake, Tanzania inapona. Kweli Mola anatupenda Watanzania hadi akamchukua akawe mpigadeki nyumba ya malaika.
 
Back
Top Bottom