Vyombo vya Habari na Waandishi ndiyo kaburi la Demokrasia

Vyombo vya Habari na Waandishi ndiyo kaburi la Demokrasia

MtuHabari

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2020
Posts
321
Reaction score
1,019
Katika kipindi hiki ambacho tunakiita cha ukombozi kutoka katika udikteta wa miaka 7 tunachokiona ni Vyombo vya habari na waandishi wa habari kutuangusha kwa kujikita kwenye habari za kijinga na mizaha badala ya kutoa nafasi za kusikia hoja za msingi na kuwapa nafasi wananchi kuipata elimu ya uraia.

Ni maajabu magazeti na Radio huoni wakiripoti kuhusu mikutano ya wanasiasa wa upinzani hata kama hoja zao ni nzito, lakini wanajikita kusifia mafanikio hewa kwa sababu za bahasha.

Kuna hoja za Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi hawajihusishi kabisa kuweka mkazo utadhani hayawahusu.

Je, bado kuna vitisho vya chini kwa chini toka serikalini? Kama hakuna nini shida ya wao kujitenga na wananchi? Au na wao yakiwafika tuwasusie kama tulivyo msusa Musiba?
 
Wapinzani Walioshindwa kujijengea hata ofisi Yao ya chama watakuwa na hoja ipi nzito?

Watanzania siyo vilaza
 
Wapinzani Walioshindwa kujijengea hata ofisi Yao ya chama watakuwa na hoja ipi nzito?

Watanzania siyo vilaza
Kuna chama cha siasa kimejijengea ofisi nchi hii kweli????, au ndio mtu ukiongwa hujizuii tena unaachia vyote?? Manake kama CCM hata vile vya wananchi imevichukua kibabe kudai vya kwao. Ebu tuangalieni yenye tija
 
Akielewa kwa majibu haya naamini atakuwa amepata tohara nzuri ya akili.
 
Back
Top Bottom