DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Ukitazama uchaguzi wa mwaka huu, utagundua kuwa vyombo vyetu vya habari vimekuwa vikiweka msisitizo mkubwa kwenye masuala ya amani na haki. Hili si jambo baya, lakini ni muhimu watambue kwamba, wakati wakihubiri amani, kuna kundi la watu ambalo limekuwa likipaza sauti kuhusu utekaji, upoteaji wa watu, na kukandamizwa kwa maandamano. Ni vyema wakakumbuka kuwa hakuna amani ya kweli bila haki.
Vyombo vya habari vina wajibu mkubwa wa kusemea wananchi, si kuisemea serikali au chama tawala (CCM). Ndiyo maana mara nyingi media huitwa the Fourth Estate yaani nguzo ya nne ya utawala. Hata hivyo, nchini Tanzania, vyombo vingi vya habari vimekuwa vikijikita zaidi kuripoti mazuri kuhusu CCM huku vikipuuzia au kuficha mapungufu yake.