GE2025 Vyombo vya Habari Tanzania Vimepoteza Dira, Watawala Wanalindwa, Wananchi Wananyamazishwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Ukitazama uchaguzi wa mwaka huu, utagundua kuwa vyombo vyetu vya habari vimekuwa vikiweka msisitizo mkubwa kwenye masuala ya amani na haki. Hili si jambo baya, lakini ni muhimu watambue kwamba, wakati wakihubiri amani, kuna kundi la watu ambalo limekuwa likipaza sauti kuhusu utekaji, upoteaji wa watu, na kukandamizwa kwa maandamano. Ni vyema wakakumbuka kuwa hakuna amani ya kweli bila haki.

Vyombo vya habari vina wajibu mkubwa wa kusemea wananchi, si kuisemea serikali au chama tawala (CCM). Ndiyo maana mara nyingi media huitwa the Fourth Estate yaani nguzo ya nne ya utawala. Hata hivyo, nchini Tanzania, vyombo vingi vya habari vimekuwa vikijikita zaidi kuripoti mazuri kuhusu CCM huku vikipuuzia au kuficha mapungufu yake.
Your browser is not able to display this video.
 
Kuna vyombo vya Habari au Propaganda Machines ?!!!

Na hili kwa sasa linaelekea kuikumba dunia nzima....
 
Ahadi ya mzigo inafanya kazi
 
Hizo ndio toilet paper alizosema Kipanya sio media.

Media ni zile zinazokemea maandamano na uchaguzi wa kiinimacho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…