May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Inakera sana kusikia chombo rasmi cha habari, kilichoaminiwa na serikali mpaka kupata leseni kushiriki kueneza upuuzi kwa lengo tu la kupata Wasikilizaji au Wafuatiliaji.
Tunaweza kuchukulia mambo kirahisi lakini amini amini nawaambia madhara yake yanaitafuna jamii taratibu na tutadhalilika.
Ni rahisi Mtu kuipuuza habari kama ataisikia kupitia Vyombo vidogo au visivyo rasmi lakini iwapo Watu wataisikia taarifa hiyo hiyo kutoka kwa Vyombo na Watangazaji wanaowaamini ni hatari sana kwa jamii.
Milard Ayo ni kati ya Vyombo vilivyofanikiwa kujijengea imani miongoni mwa jamii lakini mpaka sasa sijui ni kwa nini wanashindwa kujiweka kando kwa kusahadadia na kueneza habari za kipumbavu.
Leo utawasikia wakiripoti kuhusu mambo ya "Teleza", kesho utasikia mawe yanarushwa kutoka kusiko julikana, keshokutwa utasikia kuna moto unawaka bila kuwashwa n.k...tupo mwaka 2022 hivi kwa mwendo huo bado tutamshangaa Mtoto wako leo akihoji ni kwa nini aliyegundua Mlima Kilimanjaro au Ziwa Victoria ni Mzungu?...huenda kweli Wazee wetu walikuwepo lakini je walikuwa wanajua hata kinachoendelea au nao walikuwa kama Mbuzi tu na Nyati wasioona tofauti yoyote ya Mlima Kilimanjaro na kichuguu cha Mchwa?.
Hivi kama kweli kuna mawe yanaruka kutoka kusikojulikana (ambao ni upumbavu wa hali ya juu kuamini huo ujinga) kwa nini tusifanye kazi ya kujua ni nini kinaendelea kabla ya kukimbilia tu kuhakikisha tunashirikisha nchi nzima huo upumbavu?.
Hivi kama ni kweli kuna mawe vipi kama kuna mahali jirani labda miamba inatanuka na kusinyaa hivyo kusababisha mawe kuruka?...Hamuoni kwamba Taarifa yenu itakuwa ya kujenga kama mataitaarifu Jamii ya Kitanzania kuwa ni miamba inameguka?.
Kwa hiyo tukiri tu ya kwamba sisi ni kama Inzi tu kazi yetu kushangilia mpaka Wazungu waje watuambie kuna nini kinatokea ndio kesho na kesho kutwa Watoto wetu wakutane na hizo taarifa kwenye Vitabu vyao vya Geography?.
Tumebakia kujazana tu taarifa za kijinga kama vile vile tulivyokuwa tunaishi miaka mia kadhaa iliyopita mpaka Wazungu walipokuja na kutambulisha hata mambo ya kiasili kwani waliona tuliopo hapo hata hatuoni tofauti yoyote.
Tuache mizaha ya kujisherehesha tu kumbe kuna kundi tu la Walevi na Wavuta bangi wanarusha mawe na Vyombo vya habari mnakazana kupumbaza Watanzania wenzenu kwa bidii.