GE2025 Vyombo vya Habari vya Asili (Traditional Media) vimenunuliwa kupotosha ujumbe wa TEC?

GE2025 Vyombo vya Habari vya Asili (Traditional Media) vimenunuliwa kupotosha ujumbe wa TEC?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Wakuu

IMG_20251015_233850_461.jpg

TEC walifanya misa siku ya kumbukumbu ya kifo cha Mwl. Nyerere, na kutoa waraka wao juu ya uchaguzi wakitaka wapiga kura na wanaopigiwa kura kuangalia dhamira zao za ndani ili kuwaongoza kufanya maamuzi.

Sasa maneno hayo yamegeukaje na kumaanisha 'kubariki uchaguzi? Na ambavyo hawakutaka kujisumbua vichwa vya habari wala havikutofautiana katika kufanya upotoshaji huu, jambo linaloonesha kuwa chanzo chao ni kimoja.

IMG_20251015_233849_997.jpg

Nani anafanya upotoshaji huu ili wananchi washiriki kwenye uchafuzi huu? Ni ili kuhakikisha Samia anashinda kwa namna yeyote ile ikiwemo kupotosha ujumbe wa kanisa? Au ni wapambe wake mradi hela zinatembea wanaweza kula hata kinyesi na wasijali chochote?

Kwenye mambo kama haya huwezi kuona TCRA, wala JAB kwasababu ukweli ni kwamba wote ni wamoja katika kuhahakisha udhalimu unapita.

IMG_20251015_233850_530.jpg
Hii kwa maana nyingine inamaanisha presha inazidi kupanda kwa serikali, CCM na washirika wao juu ya Watanzania kugomea uchaguzi. Yaani safari hii uchaguzi umekataliwa na kila mtu, sasa wanatapatapa kufeki kwa namna yoyote ile kuonesha kukubalika!

Mwendo ni ule ule, lazima wakae safari hii! Watanzania wa leo sio wa jana!
 
Si mpo kwenye mapambano?
Kila mtu anaonyesha kile anachokiweza...

Ukitaka kujua kuwa serikali haitanii, kesho tu eneo lako la kazi au palipo na watu we simama useme sijui tarehe 29 oct unaandamana! Hapo utajua kuwa maandamano si mchezo..

Anyway RC au TEC si msemaji wa watanzania kuhusu kupga kura ama kutokupga kura..

kikatiba hawana mandate yoyote kuamua chochote kuhusu katiba.

katiba si liturgy!
 
Umeandika nini hapa?🤔🤔
 
Wakuu

TEC walifanya misa siku ya kumbukumbu ya kifo cha Mwl. Nyerere, na kutoa waraka wao juu ya uchaguzi wakitaka wapiga kura na wanaopigiwa kura kuangalia dhamira zao za ndani ili kuwaongoza kufanya maamuzi.

Mwendo ni ule ule, lazima wakae safari hii! Watanzania wa leo sio wa jana!
Bwana wetu Yesu Kristo, alitufundisha tumpe Mungu yaliyo ya ki Mungu na tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari. Uchaguzi ni la Kaisari, Kanisa lina wajibu kuwapa warming wake uhuru wa kuchagua hivyo kubariki Uchaguzi Mkuu uwe huru, wa haki na wa Amani.
Hata ile novena, tulifunga na kuomba, kuombea Uchaguzi.
P
 
Askofu wa Kanisa Katoliki hakuubariki Uchaguzi.

Amesema haelewi kabisa mambo yanavyokwenda---- Uchaguzi unavyokaribia,watu wanazidi kutekwa. Amesema wapiga kura waamue wenyewe watapiga kura vipi.

At least tunaweza kusema Kanisa Katoliki linabariki Uchaguzi.

Rafiki zetu wengine wanasema Oktoba 29 hautakuwepo Uchaguzi.

Kwa hiyo askofu ameubariki Uchaguzi,bila kukusudia.

Uchaguzi probably utakuwa very peaceful. Labda watu wachache watataka kuleta fujo, lakini watazuiwa.
Imefikia mahala mpaka wengine wanatoa ushauri jinsi ya kuitengeneza Molotov cocktail,bomu la chupa na petroli, lakini hawakamatwi.

Sidhani kama inawezekana kuuzuia Uchaguzi, and I don't think it is necessary to do so.

Lakini I don't want to pose as an advisor.

Advising people is risky business. Ushauri wako ukiwaponza watu,basi unakosa haki ya kushauri.

Lakini what do you do with such people ambao wanasema maandamano yanaruhusiwa na Katiba and yet wanasema vituo vyote vya mafuta vinapaswa kuchomwa moto? Kuchoma moto vituo vya petroli pia kunaruhusiwa na Katiba?

Manung' uniko ya utekaji siyapendi sana. Polepole kila mtu amemsikia Polepole akisema anataka kumyonga Rais Samia.

And yet Polepole akitekwa Mafwele anatakiwa kuomba msamaha.

Lakini yule Askofu hajaubariki Uchaguzi. Pia hajaulaani Uchaguzi. Kwani,kama haumpendezi,there is nothing he can do about it.

We are all spectators here.

Lakini utajiri wa hawa viongozi wengine unatisha. There comes a point wakati hata Shetani anakasirika wafuasi wake( Shetani) wakizidisha uovu
 
Mainstream media na bloggers wakubwa wote ndani ya TZ wamegeuzwa kuwa chawa(puppets) either kwa kutishwa au kwa rushwa plus ahadi za 'kuangaliwa vizuri' kwenye kodi wanazopaswa kulipa.
 
Back
Top Bottom